Godwin Makomba,mmoja ya viongozi walihama Chadema
Chama
kipya Cha Aliance for Change and Transparent (ACT), Tanzania kimenza
kuonesha makucha yake mkoani Shinyanga baada ya viongozi wa Chadema
kujivua nyadhifa zao na kuhamia chama hicho kwa madai kuwa rushwa
imetawala ndani ya Chadema
Waliojivua
nyadhifa zao na kujiunga na ACT ni Godwin Makomba, aliyekuwa katibu wa chadema jimbo
la Solwa katika halmashauli ya wilaya ya Shinyanga vijijini na mjumbe wa
mkutano mkuu wa wilaya,Merikioli Sebastiani, aliyekuwa katibu mwenezi wa kata ya Kambarage, Samweli
Dalla aliyekuwa mwenyekiti wa Chadema wa kata ya Kambarage wilaya ya Shinyanga Mjini na Samweli
Rafael aliyekuwa mhasibu wa kata ya Kambarage.
Wamesema
wameamua kujiunga na ACT kutokana na
Chama chao cha awali (Chadema),kutowatendea haki na kutozingatia
Demokrasiana viongozi wa ngazi za juu kudharau viongozi wa ngazi za
chini na kwamba baadhi ya taarifa za kiofisi zinazowahusu zilikuwa
haziwafikii.
“Tumeamua kujivua uanachama kwani viongozi wa ngazi ya juu wamekuwa
wakikemea rushwa na kudai demokrasia hasa kwenye uchaguzi wa ndani
ya chama uliopita baadhi ya majina ya watu yalichakachuliwa manispaa
na kuingizwa majina ambayo hayakutakiwa kwa hilo tutaonekana
wanafiki kwa kutoendana na kauli zinazotamkwa”waliiambia Malunde1 blog
Wamesema baadhi ya walioenguliwa bila sababu yoyote kwa mizengwe na
kupitia kura za red-brigde ni aliyekuwa mwenyekiti wa wilaya wa
chama hicho na diwani viti maalumu Siri Yasin na diwani wa kata ya
Kambarage (Chadema) ,aliyekuwa katibu wa mkoa na baraza
la wazee taifa Nyangaki Shilungushela.
0 comments:
Post a Comment