Showing posts with label UDAKU. Show all posts
Showing posts with label UDAKU. Show all posts


Mapenzi bhana! Baada ya kutoka
kimalavu na kumwagana na mwanadada
mwenye mvuto Bongo, Wema Isaac Sepetu
‘Beautiful Onyinye’ kisha kuangukia
kwenye ‘utamu’ wa penzi la mwanamama
anayekimbiza Uganda, Zarinah Hassan
a.k.a Zari au The Boss Lady, Nasibu Abdul
‘Diamond Platnumz’ ameamua kuanika siri
tano za kilichomvutia kwa staa huyo
gumzo Afrika Mashariki.
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’
akiwa na mwanamama anayekimbiza
Uganda, Zarinah Hassan a.k.a Zari au
The Boss Lady.
Akizungumza katika mahojiano maalum
katika ofisi za gazeti hili, Bamaga-Mwenge
jijini Dar hivi karibuni, bila kupepesa
macho au kuuma maneno baada ya
kuulizwa kinagaubaga juu ya ukaribu wake
na Zari, Diamond au Dangote hakutaka
kuficha, akaamua kuweka mambo yote
hadharani.
MATANGAZO
Alifunguka: “Mimi ni mwanamuziki
mkubwa na mwenye heshima, wakati
mwingine natakiwa kuwa na akili ya kuwa
na uhusiano na watu ambao watakuwa
msaada kwangu pia.
“Siwezi kuwa karibu na mtu ambaye
hataniongezea kitu chochote kile. Baada ya
kujitangaza sana Tanzania, nikahamia
Kenya ambapo nilikuwa karibu na
mwanadada Avril. Ukaribu wangu kwake,
ukanifanya Kenya kutambulika.
“Baada ya kukaa kwa muda, nikataka
nitambulike na Uganda pia, unafikiri
ningefanya nini? Nikaliteka soko lao kwa
kuwa karibu na mrembo Zari.
“Kweli nimefanikiwa na hata siku ya shoo
yake (Desemba 18, mwaka huu nchini
Uganda), ilikuwa ni balaa kiasi kwamba
sikuamini kilichokuwa kimetokea, watu
walikuwa nyomi ile mbaya. Mbali na kuwa
mwanamuziki mkubwa, bado nahitaji
kujitangaza zaidi.”
Zari na Diamondi wakibusiana
kimahaba.
MSISIMKO
Sababu ya pili aliyoitaja ni kwamba Zari
ambaye ni mama wa watoto watatu ana
msisimko wa aina yake tofauti na ‘mashori’
wengine aliwaowahi kuanguka nao
dhambini.
“Hakuna mwanaume anayependa kukaa na
msichana asiyekuwa na msisimko wa
kimapenzi. Hebu fikiria umekaa na
mwanamke mwenye umbo kama la
mwanaume, utapata msisimko gani hapo?
Lakini mcheki mtoto alivyong’aa,
anameremeta, mtoto yupo bomba, ukikaa
karibu yake tu utagundua kwamba umekaa
na msichana mwenye mvuto ambaye kila
wakati atakufanya kuwa bize
kumwangalia.”
BIASHARA
Sababu ya tatu aliyoitaja Diamond ni
kwamba mwanadada huyo yupo vizuri
kibiashara.
“Ninaangalia fedha, ili biashara zangu
ziweze kupiga hatua sina budi kukaa
karibu na mfanyabiashara mwenzangu
(Zari) kwa ajili ya kushauriana biashara
ziende vipi.
“Yeye (Zari) ni mkongwe katika biashara,
kuwa karibu naye naamini nitajifunza
mambo mengi sana.
Amekuwa muwazi kwangu na amenipa
mianya mingi ya kufanya biashara, lakini je,
nisingekuwa karibu naye, michongo hiyo
ningeipata vipi?”
Zari na Diamondi wakiwa kwenye pozi.
UZURI
Sababu ya nne ya kuwa na Zari, Diamond
alidai kwamba mwanamama huyo ni mzuri
kupita maelezo.
Alifunguka: “Mimi ni mwanamuziki
mkubwa, watoto wazuri wananipenda kwa
hiyo kama ningefanya uamuzi wa kuwa na
mwanamke asiyekuwa mzuri, maneno
yangeanza kusikikasikika na isingekuwa
poa. Mbali na kuwa mfanyabiashara,
kumtumia kama msaada wa kunitangaza,
lakini Zari ni mzuri bwana. Ni mwanamke
ambaye kwa kumwangalia tu, unaweza
kusema kwamba haujawahi kukutana na
mwanamke mzuri kama yeye.
ANAJITAMBUA
Sababu ya mwisho aliyoianika Diamond ni
kwamba Zari yupo vizuri kichwani kwa
maana ya kujitambua tofauti na wanawake
wote aliowahi kutembea nao.
Mwanadada mwenye mvuto Bongo,
Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’.
“Nimekuwa na wanawake tofautitofauti
lakini kwa Zari, ni mwanamke mwenye
hekima na anajitambua sana. Si
mzungumzaji kivile na huwa anapenda
kufanya vitendo kuliko maneno.
“Anajua ni kipi anatakiwa kufanya na akili
yake ameielekezea kwenye fedha zaidi.
Hapendi masihara na fedha, anapenda
kujitoa na ni mchakarikaji sana. Nampenda
mwanamke wa hivyo kwa kuamini
kwamba atanifanya nijitume zaidi.”
AWACHAMBUA JOKATE, WEMA NA
PENNY
Diamond alipoulizwa juu ya kasoro za
warembo wakali Bongo aliowahi kutoka
nao wakiwemo mrembo Jokate Mwegelo
‘Kidoti’, Wema na mtangazaji wa Radio E-
FM, Penniel Mungilwa ‘Penny’,
aliwachambua mmoja baada ya mwingine
na kuhitimisha kuwa ni wazuri lakini
hawamfikii Zari.
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
UTAMBULISHO KESHO DAR LIVE
Mbali na kuziweka wazi sifa za Zari, jamaa
huyo alidai kwamba atamtambulisha rasmi
kwa Wabongo kesho usiku kwenye Uwanja
wa Kimataifa wa Burudani wa Dar Live,
Mbagala jijini Dar atakapokuwa
anaangusha burudani ya kibabe katika
Tamasha la Wafalme akiwa na mfalme
mwenzake, Mzee Yusuf na wakali wengine
kibao kwa kiingilio cha shilingi 10,000/=
kwa kawaida na shilingi 20,000/= kwa
V.I.P.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI LIKE PAGE YETU HAPO PIA SHARE STORY NA RAFIKI ZAKO
Wednesday, December 24, 2014

Usiku wa juzi tarehe 18, jiji la Kampala nchini
Uganda lilipambwa na “EVENTS” mbili mkubwa
kwenye upande wa buruani ambazo ni Show kubwa
ya mwnamziki Jose Chameleone iliyofahamika
kama 1Man Show Million na Pati ya mwanamama
Zari iliyofahamika kama Zari All White Ciroc Party.
Mwigizaji Wema Sepetu na mwanamziki Diamond
Platnumuz wote walitua nchi humo na kugawana
matukio hayo kama ifuatavyo;
Wema Sepetu ambae anadai ni amekuwa shabiki
mkubwa wa masanii Jose Chameleone alitokea
nchini Ghana na kutua jijini Kampala kuhudhuria
show ya mwanana mziku huyo ambayo ilifanyika
Serena Hotel.
Wakati Diamond Platnumz ambae kwasasa ana “Le
Project” na mwanamama Zari alihudhulia pati ya
Zari kama “Special Guest”.
Baadhi ya watu wamechukulia kitendo hiki ni kama
mwanadada Wema “Amepaniki” hivi, Huku wengine
wakisema kuwa Wema ana uhuru wakufanya kile
anachokitaka bila ya kuhofia watu watasemaje.
Jambo hili halijatokea kwa bahati mbaya kwani wiki
kadhaa zilizopita, Diamond alipoonyesha kum-
support Zari kwenye pati yake,Wema nae alibuka na
kum-support Jose. Kama unavyoona hapa chini.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI LIKE PAGE YETU HAPO PIA SHARE STORY NA RAFIKI ZAKO
Saturday, December 20, 2014



gene
Mwigizaji wa Nollywood Genevieve Nnaji amefunguka kuhusu hatma ya maisha yake ya ndoa na kuelezea ni kwa nini hana haraka ya kuingia katika maisha hayo kwa sasa.
Kwa mujibu mahojiano aliyofanyiwa na Gazeti la Vanguard la Nigeria amesema ndoa sio kitu cha kukurupuka na kinahitaji muda zaidi katika kujipanga na kutekeleza.
“Endapo nitaolewa,natamani sana nidumu kwenye ndoa yangu na kudumu kwake najua si kazi ndogo inahitaji uvumilivu mkubwa,nafahamu unapoingia unatakiwa kufahamu kile ni kifungo cha moja kwa moja na mwenzako ndio wa kufa na kuzikana hivyo tunapaswa kutambua kuna shida na raha zake na pia tunapaswa kujifunza kusamehe na kusahau endapo tunakwazana na wenza wetu,”alisema Genevieve.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI LIKE PAGE YETU HAPO PIA SHARE STORY NA RAFIKI ZAKO
Sunday, December 14, 2014


1
Muimbaji wa Mduara, AT ameshinda kesi iliyokuwa ikimkabili na
iliyofunguliwa na mganga wa jadi kwa madai kuwa hakulipwa fedha baada ya
kumpandisha nyota na kupata mafanikio mengi.
Akizungumza XXL ya Clouds FM, AT amesema uamuzi huo ni faraja kwake kwakuwa ilimfanya ashindwe kufanya mambo yake.
“Hukumu imetolewa kama dakika tano zilizopita lakini tulikuwa
tumefika toka asubuhi saa mbili, kwahiyo itambulike kuwa AT ni msanii
huru,” alisema.
“Namshukuru Mungu kwa uwezo wake mkubwa kuonyesha
waganga wa jadi kwamba yeye yupo na kazi yake ni kubwa na haingiliwi na
mtu.”
“Nimeshinda kwa kishindo kama CCM na sasa najisikia faraja sana, kwa
sababu kiukweli kabisa nilikuwa nashindwa kufanya kazi zangu za muziki
hata kama nyimbo nzuri basi nahisi hata hii nyimbo ikienda hata kama
itafika nitaambiwa nimelogezea hali ya kuwa sio kweli,” aliongeza.
“Pia hata mashabiki zangu nilikuwa nimewaangusha, sasa hivi ndo muda
muafaka ndio maana hata nilijifungia ndani nilikuwa nakosa uhuru wa
kuishi. Kwahiyo hii kesi imeathiri vitu vingi imenitia nuksi, naacha
huu mwaka uishe ili nijipange na mwaka ujao.”
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI LIKE PAGE YETU HAPO PIA SHARE STORY NA RAFIKI ZAKO
Sunday, December 14, 2014

Anajulikana kwa jina la Naisula
Lesuuda ambaye aliwahi kuwa
mwandishi wa kituo cha Tv kenya cha
KBC lakini kwa sasa ni senetor kutoka
kenya ambaye ni mzuri kuliko
wabunge wote wanawake nchini
Kenya picha zake hizi hapa chini!

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI LIKE PAGE YETU HAPO PIA SHARE STORY NA RAFIKI ZAKO
Saturday, December 13, 2014

Jumapili ya Des 7 ni siku iliyochukua headline
kwenye mitandao baada ya Davido kuwakwaza
watanzania kwa kile alichokiandika kwenye
twitter.Baada ya Mwakilishi kutokea Tanzania
Idris Sultan kutangazwa kuwa mshindi wa Big
Brother Africa Hotshots.
Mengi yamezungumzwa na watu,lakini Des 11
mshindi wa Big Brother Africa Hotshots,Idris
Sultan alipata nafasi ya kuzungumza na
vyombo vya habari mbalimbali. Miongoni mwa
maswali aliyouliza ilikuwemo ile ishu ya
Davido.
Mwandishi: Idris ukiwa kama mshindi wa BBA
unazungumziaje ujumbe wa Davido
uliowakwaza watumiaji wa mitandao?
Idris Sultan: “ Kwanza ningependa kusema
nahisi ilikuwa ni utani kwasababu mwishoni
mwa ile sentensi kumbuka kuna alama ya utani
yaani ‘Lol’ sasa nimeshangashwa kuona watu
wanaanza kuhisi vibaya kuwa ni dongo kwetu
hapana.
“Ningewataka watanzania pamoja na Davido
tusiingie kwenye migogoro isiyokuwa na msingi
sisi sote ni bado vijana tunatakiwa kujitangaza
na kupeana support hata vizazi vinavyokuja
vijifunze vitu vizuri kutoka kwetu ikiwemo
Upendo na Amani kati ya Tanzania na
Nigeria.”
Hizi ni baadhi ya picha kutoka kwenye
mkutano huo
Mshindi wa Big Brother 2014,Idris Sultan
akisisitiza jambo wakati akiongea na waandishi
wa habari (hawapo pichani) katika hoteli ya
Hyatt Regency,Jijini Dar es salaam .
Idris akizungumza.
Aliyekuwa Mshiriki mwenza wa Idris
Sultan,Irene Laveda akizungumza machache
kwenye Mkutano huo.
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya MultiChoice
Tanzania,Barbara Kambogi akizungumza jambo
wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari
jijini Dar es Salaam.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI LIKE PAGE YETU HAPO PIA SHARE STORY NA RAFIKI ZAKO
Friday, December 12, 2014

KWA mara ya kwanza baada ya kutua Bongo,
Mshindi wa Shindano la Big Brother Hotshort
( 2014) , Idris Sultan amemfungukia mwigizaji
Elizabeth Michael ‘Lulu ’ na kudai ni rafiki yake
wa karibu .
Mshindi wa Shindano la Big Brother
Hotshots 2014, Idris Sultan.
Kabla mshindi huyo hajakanyaga Bongo , Lulu
alishambuliwa mitandaoni baada ya kujinadi
kuwa na urafiki wa karibu na Idris lakini kwa
kauli hiyo, imeonesha dhahiri wawili hao ni
marafiki wa kweli tofauti na mitazamo ya
wadau mitandaoni .
Mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu ’ .
“ Lulu ni rafiki yangu wa muda mrefu , hakuna
kingine zaidi ya urafiki . Tutaendelea kuwa
marafiki hata baada ya ushindi huu,” alisema
Idris , juzi alipokuwa kwenye mkutano wa
waandishi wa habari kwenye Hoteli ya Hyatt
Regency Dar es Salaam ( The Kilimanjaro ).

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI LIKE PAGE YETU HAPO PIA SHARE STORY NA RAFIKI ZAKO
Friday, December 12, 2014

MASTAA wana mambo! Mtoto mzuri Bongo Movies,
Elizabeth Michael ‘Lulu’ ametoa kali ya aina yake
kwa kusema kamwe hatumii nguvu nyingi kwenye
mapenzi kwa sababu yanapoteza muda bila
sababu za msingi bora nguvu zake azitunze hadi
pale atakapokuwa akijifungua.
Mtoto mzuri wa Bongo Movies, Elizabeth Michael
‘Lulu’ akipozi.
Akimwaga cheche mbele ya mwanahabari wetu,
Lulu alisema siku hizi wanaume wengi
wanawafanya wasichana watumie nguvu kutetea
penzi kutokana na migogoro isiyokuwa na msingi.
“Bora nguvu zangu nizihifadhi za kuendea leba
kuliko kuzipoteza katika mapenzi kwani hayo
mambo yamepitwa na wakati kabisa,” alisema
Lulu.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI LIKE PAGE YETU HAPO PIA SHARE STORY NA RAFIKI ZAKO
Wednesday, December 10, 2014

Mshindi wa Big Brother ‘hotshots’ 2014,
Idris Sultan kutoka Tanzania aliyekuwa
akituwakilisha ndani ya mjengo huo.
KAMA TULIVYOITOA TATHMINI MAPEMA
ASUBUHI YA LEO KUWA TANZANIA INA
90% ZA USHINDI! NDIVYO ILIVYOKUA!
Mshiriki kutoka Tanzania aliyekuwa
akituakilisha  ndani ya mjengo wa Big
Brother ‘hotshots’ , Idris Sultan ameibuka
kidedea katika shindano hilo usiku huu na
kunyakuwa kitita cha dola 300,000 (Sawa
na 510,186,000).
Fainali za Big Brother ‘hotshots’ zilianza
saa 2 :00 Usiku huku Idris akiwaongoza
wenzake saba ambao ni Tayo (Nigeria), JJ
(Zimbabwe), Nhlanha (Afrika Kusini), Sipe
(Malawi), Butterfly (Zimbabwe), Ma mbea
(Ghana) pamoja na Macky2 wa Zambia.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI LIKE PAGE YETU HAPO PIA SHARE STORY NA RAFIKI ZAKO
Sunday, December 07, 2014

Mkanda wa ngono unamuonesha mfanyabiashara
wa Uganda, Zarinah Tlale maarufu kama Zari the
Bosslady akifanya mapenzi na mwanaume
asiyejulikana umesambaa.
Picha za Zari akivunja amri ya sita kutoka kwenye
mkanda huo zimechapishwa kwenye gazeti la
udaku la Red Pepper la Uganda.
“For exclusive pictures and a clear description of
how Zari moans in bed, Please hurry and Grab Red
Pepper copies of Friday and Saturday from the
nearest vendor,” umeandika mtandao huo.
Zari ambaye hivi karibuni amekuwa na uhusiano na
Diamond Platnumz, amesema mkanda huo
umetolewa kwa makusudi ya kumharibia biashara
zake.
Kupitia Instagram, Zari amezungumzia kitendo
hicho kwa kirefu:
Dearest friends, my fans all over the world,
relatives and well wishers, as you may be or may
not be aware, the print media in Uganda is awash
with stories infringing on my fundamental
inalienable human rights by attacking my modesty
both as a woman and a mother to the utter
prejudice of my private life and family. The clear
motive of such publication is undoubtedly to deter
and/or downplay my tireless efforts in my
preparations for The Zari All White Party slated for
18/12/14 which to a large extent has rubbed some
of my detractors the wrong way. I have no doubt in
my mind that the pictures that appeared in today’s
Red Pepper issue were leaked by someone for their
own selfish motives. Be that as it may, I would like
to affirm that what goes on in my private life is
absolutely my business that has no reason
whatsoever to find it’s way in the public realm.
Privacy to/for/of a person is not a right granted by
anyone, but it’s inalienable. I am therefore steadfast
in my resolve to hold the Zari All White Party for all
my fans and friends in Uganda. And whilst I explore
the option of seeking with a view of taking legal
action against the perpetrators/detractors and/or
publishers, I want to assure all my family, fans and
friends again to disregard such hurtful reports
aimed at scoring cheap social points. Lastly, I call
upon one and all to attend the All White Party as
there’ll be incredible performances from various
artists including Diamond Platinumz, whose
attendance is confirmed. I’d love to see you there,
I’ll be there to welcome you all and God willing, we
shall have a great time like we always do. Bless

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI LIKE PAGE YETU HAPO PIA SHARE STORY NA RAFIKI ZAKO
Friday, December 05, 2014

Hizi ndio ndio picha za mwanamke alio katwa ziwa na mumewe kisa wivi wa mapenzi baada ya kumuisi anatoto na mtu

((  Bofya hapa kuona ila zinatisha"")!!!

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI LIKE PAGE YETU HAPO PIA SHARE STORY NA RAFIKI ZAKO
Friday, December 05, 2014

B Assemblies of God jijini Dar, Dk. Getrude
Rwakatare (pichani) amefunguliwa mashitaka
katika Kituo cha Polisi Wazo Hill kwa uharibifu wa
mali inayodaiwa ina thamani ya shilingi milioni 20.
Bw. Grayson Justine anayelalamika kuvunjiwa
nyumba yake na Mch. Getrude Rwakatare.
Taarifa zilizopatikana katika kituo hicho zenye
Jalada la Kumbukumbu WH/RB/9029/2014
UHARIBIFU WA MALI na kuthibitishwa na
mlalamikaji aliyejitambulisha kwa jina la Grayson
Justine, zinaeleza mchungaji huyo alivunja nyumba
ya Grayson kwa greda hali iliyomfanya mmiliki
huyo kuzimia na kulazwa Zahanati ya Mico iliyopo
Wazo Hill baada ya presha kupanda.
Katika mahojiano na waandishi wetu katika Ofisi za
Global Publishers, Bamaga- Mwenge, Dar wiki
iliyopita, Grayson alikuwa na haya ya kusema:
Nyumba ya Bw. Grayson wakati wa ujenzi.
“Kiwanja nilichojengea nyumba nilikinunua kwa
Jumanne Rajab, Agosti 24, 2011 na makubaliano
yalifanyika kwa kuandikishiana Ofisi za Serikali ya
Mtaa wa Bunju ‘B’ na kila mmoja alikuwa na
mashahidi wake.
“Kutokana na kuchoka katika kupangisha, niliamua
kuchukua mkopo wa shilingi milioni 20 kazini ili
nijenge haraka na kuhamia, ujenzi ulianza
Septemba 21,  mwaka 2013 mpaka kufikia mwezi
huu (Novemba) nilibakiza kupaua na nilitarajia
kuhamia mwanzoni mwa mwaka kesho.
Mabaki ya matofali ndani ya uzio wa Nyumba ya
Bw. Grayson Justine iliyobomolewa kwa greda.
“Baadaye nilikwenda Moshi kwenye msiba wa
baba, niliporudi Dar nilimaliza siku moja tu,
nikaripoti kazini. Nikiwa kazini Novemba 11,
mwaka huu nikapigiwa simu na jirani kwamba
nyumba yangu inabomolewa na greda, alifikiri
kwamba nimeshaonana na Mchungaji Rwakatare
na kukubaliana naye.
“Nilikwenda kule, kufika nikakuta hakuna jengo!
Nilidondoka chini, sikujua kilichoendelea, nilipoteza
fahamu, nilijitambua nikiwa Zahanati ya Mico.
“Kinachoniumiza sana ni kitendo cha kuvunjiwa
nyumba yangu bila kushirikishwa, bora hata
angenifungulia mashitaka kama anaona nilivamia
kikwanja chake.”
“Yeye ana uwezo, ana ghorofa ya zaidi ya shilingi
bilioni moja iweje anionee na kunivunjia mimi
maskini niliyejenga kwa fedha za mkopo?
“Kituo cha polisi nilifika karibu mara nne lakini
mpaka leo hii sijapewa mpelelezi wala hawajafika
eneo la tukio, nataka sheria ichukue mkondo
wake.”
Mwandishi alifika katika eneo la tukio na
kushuhudia kifusi kinachodaiwa kuwa ni iliyokuwa
nyumba ya Grayson iliyovunjwa na imezungushiwa
ukuta na geti kupigwa kufuli.
Hata hivyo, Uwazi lilifika katika Ofisi za Serikali ya
Mtaa wa Bunju ‘B’ na kuonana na mtendaji
Abdallah Mkeyenge ambaye alikiri kuwepo kwa
mvutano baina ya watu hao.“Hii barua ya
makubaliano ya kuuziwa Grayson kiwanja
inaonekana imetoka ofisini hapa lakini mimi kipindi
hicho nilikuwa sijahamia ofisi hii.
Jumba la kifahari la Mch. Getrude Rwakatare.
“Ninachokumbuka kuna kipindi Mchungaji
Rwakatare alikuja na milioni tano kuwapa Grayson
na mtu mwingine yaani kuwapoza lakini walikataa
kuzichukua,” alisema mtendaji huyo.
Mchungaji Rwakatare alipopigiwa simu kuhusiana
na madai hayo alisema yupo bungeni hivyo
alimwagiza msaidizi wake, Jerad Abeid
kuzungumzia sakata hilo ambapo alisema eneo hilo
mchungaji analimiliki tangu mwaka 2005 na hati
ziko ardhi Wilaya ya Kinondoni. Alibomoa nyumba
ya Grayson akijua ni eneo lake la siku nyingi.
“Unajua katika maeneo hayo kuna watu walikuwa
wakishirikiana na ofisi za mtaa kuuza kiwanja cha
mchungaji kwa siri na tayari watu wanne
walishauziwa lakini walikuwa hawajajenga,
mchungaji aliamua kuwapoza kiubinadamu na
wameshaondoka bado watu wawili akiwemo huyo
Grayson,” alisema Jerad.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI LIKE PAGE YETU HAPO PIA SHARE STORY NA RAFIKI ZAKO
Wednesday, December 03, 2014

Dada wa hiari na Mapenzi wa Miss Tanzania 2006,
Wema Sepetu ambaye hakutaka kuliweka wazi jina
lake amevunja ukimya kutokana na kile alichokiona
kuwa ni mateso ya kujitakia anayoyapata Wema
Sepetu kutokana na kusumbukia Pnezi la
mwanamuziki mkubwa wa Bongo fleva Nasibu
Adbul maarufu kwa jina la Diamond Platinumz.
Kupitia wakala wake wa amani dada huyo
alifunguka kama ifuatavyo;
Najua wewe ni mrembo
sana, una exposure
kubwa na una pesa,
sawa wanasema
mwanamke bila
mwanaume
haiwezekani ila kwa
mimi naona
inawezekana. Jana
nimekuona sehemu
fulani Kinondoni
Umelewa sana sana..
Hivi unadhani pombe
ndio suluhisho la
matatizo yako? Tena unakunywa mipombe mikali
halafu mwanamke, Hicho kizazi kitapona kweli kwa
staili hiyo?Nakupa siri mdogo wangu wewe una
nafasi ya kuwa na mwanaume yeyete duniani, na
sio uchafu wa manzese huu unaokupata paka kila
kikwapa cha mwanamke. Kama ungeweza hebu
ondoka Tanzania japo kwa miezi sita nenda kakae
nje kama ulivyofanya kipindi kile ulivyoachana na
yule mla unga ukirudi utakuwa mpya umeweza
kukaa mbali na huyi dom* na utaona umeweza
kuishi bila yeye. Hebu jaribu kukaa bila mwanaume
uone kama haiwezekaniki, jaribu kubadili aina ya
wanume unao date nao. Date watu wa nje ya nchi
uone kama yataendelea haya haya au utaendelea
kuvaa sare za harusi za wenzio huklu pete
uliyovalishwa mwaka 47 ikitopata kutu kidoleni
mwako. Imefika stage watu wanakuona wewe
Kigodoro cha kukimbilia pale magodoro yao
yanapoingua kunguni. Wafungie vioo hao fanya
yako. Anzisha kitu cha kuku keep-busy acha
Pombe ikiwezekana hata zile company za pombe
zikimbie.
Wewe ni mdogo sana
sana kunywa mipombe
ati stress za mapenzi
utajipatia maradhi ya
figo
ungali mdogo. Labda
kama mwenzetu
wataka kufa kesho
tuambie tukuwekee
order ya mi-dompo mia
kila siku nasisitiza sana
jaribu kubadili aina ya
wanaume unaotoka
nao. Acha wanaume za
watu nenda nje jipatie
mkaka au mzungu
kama dadaako
alivyofanya katulia. Date mtu wa mbali na kwenu wa
hapa hakuna wa kukuoa watalutumia kujipatia
majina hawakupendi Wema. Ona wenzio mamisi
wameshatengeneza familia zao wewe bado huelewi
na umri unasonga mbele. Kibaya zaidi mdogo wangu
una mwili mbaya wa kuzeeka haraka na hivyo
mipombe ndio kabisa. Najua inaumiza hii ila
ukinisikia utasema asante.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI LIKE PAGE YETU HAPO PIA SHARE STORY NA RAFIKI ZAKO
Tuesday, December 02, 2014

WAKATI mabinti wengi hasa mastaa wa Bongo wakijuta baada ya picha zao za utupu walizopigwa na wapenzi wao kuvuja, kwa msanii mrembo aliyepamba video ya wimbo wa Bongo Fleva uitwao Jambojambo wa msanii Steve R&B, Aisha Firozi ‘Sapna’ ni kawaida kwani hujifotoa mwenyewe.
Chanzo makini kimewasilisha ‘folda’ lenye picha za kutosha za mrembo huyo akiwa mtupu huku kikieleza kwamba ni mchezo wake kujipiga mwenyewe picha hizo.
Kwa sharti la kutochorwa jina lake gazetini, chanzo hicho ambacho kipo aribu na Sapna kilisema: “Yule ni mtu wangu wa karibu sana, lakini tabia yake kwa kweli huwa siipendi kabisa. Anajipiga picha chafu mwenyewe, kwake ni starehe kubwa, huwezi kuamini.” Kikiendelea ufunguka zaidi, chanzo hicho kilipasha kuwa, picha hizo amejipiga hivi karibuni nyumbani kwa rafiki yake aitwaye Doreen, Tabata - Magengeni jijini Dar es Salaam, ambapo alikuwa akiishi naye.
GONGA HAPA KUMSIKILIZA SAPNA
Ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni; Sapna alipopigiwa simu na paparazi wetu na kuelezwa kuhusu kunaswa kwa picha hizo, kwanza alishangaa lakini akakiri kuzitambua.
“Hizo kweli ni picha zangu na nilijipiga mwenyewe sasa sijui wewe umezipataje na zimefi kaje huko kwenu? Mimi nilipiga kwa masilahi yangu mwenyewe, huwa natamani sana kujiangalia jinsi umbo langu lilivyo, ndiyo maana niliamua kujipiga na si vinginevyo.
“Kila mtu na maisha yake na mimi sikuwa na dhamira mbaya kujipiga picha hizo zaidi ya kujiangalia tu nilivyo,” alisema Sapna

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI LIKE PAGE YETU HAPO PIA SHARE STORY NA RAFIKI ZAKO
Saturday, November 29, 2014


Jina la Penny limo katika orodha ya mastaa waliowahi kuwa na uhusiano na msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’. Jina lake kamili ni Penniel Mwingilwa. Huyu ni Mtangazaji wa Radio Efm ya jijini Dar.


Wiki hii yuko hapa kujibu maswali ambayo waandishi wetu Imelda Mtema na Hamida Hassan walimuweka mtu kati.Ijumaa: Mambo Penny, naona sasa hivi una gari nyingine, ile Toyota Brevis ambayo mpenzi wako wa zamani Diamond alikununulia iko wapi?


Penny: (Kicheko)...kwa kweli namshukuru kwa kuninunulia ile gari ila sasa hivi siko nayo, nimeamua kubadilisha, si unajua mtu lazima uende na wakati?

Ijumaa: Mara ya mwisho kupanda daladala ilikuwa lini?

Penny: Nakumbuka ilikuwa mwaka 2008. Nilipoanza tu kazi ya utangazaji, nilipopanda daladala watu walikuwa wananishangaa sana nikaona hiyo siyo poa, nikawa napanda teksi.


Ijumaa: Ulikuwa na Diamond mkaachana, hebu tuambie kwenye maisha yako ungependa umpate mwanaume wa aina gani?Penny: Kwanza awe mchamungu, pili anithamini lakini pia awe mtu muelewa. Yaani ajue ni wakati gani wa kufanya maamuzi sahihi na awe tayari kunisikiliza.


Ijumaa: Nini ambacho kinakukwaza sana na hukipendi kabisa?

Penny: Ni watu kuniongelea tena kwa mambo ambayo hawayajui kuhusu mimi. Nakerwa sana na wanaofanya hivyo.Ijumaa: Ukiwa katika ‘stress’ au mtu kakukwza na kukukosesha amani, kipi ambacho huwa unakifanya kurudisha amani yako?

Penny: Nikiwa katika hali hiyo breki ya kwanza ni kanisani. Pale kwenye Kanisa la St. Joseph pembeni kuna kakanisa kadogo.Kwa hiyo nakwenda pale, nasoma Biblia na kusali kwa muda wa saa sita hivi kisha nikiondoka hapo nakuwa sawa.


Ijumaa: Muda wa kuolewa ukifika na mwanaume akaja kwenu na ukatakiwa utamke mwenyewe mahari yako, ungetaka mahari ya shilingi ngapi?Penny: Sina makuu, nitamtaka mwanaume huyo ampe baba yangu juzuu na msahafu halafu mama yangu apewe Biblia. Kama kutakuwa na pesa kidogo tutaipeleka kwa watoto yatima.


Ijumaa: Mastaa wengi wa kike wanadaiwa kutojua kupika, wewe hili likoje kwako?

Penny: Kitu ambacho nitamshukuru mama yangu siku zote ni kunifundisha kupika. Najua kupika vitu vingi sana tena vinakuwa vitamu mno, kasoro ugali ndiyo unanishinda ila najitahidi kujifunza.

Ijumaa: Umeanza kujitegemea ukiwa na umri mdogo, vipi unajilindaje na vishawishi vya wanaume?

Penny: Wakati naanza kupanga tulikaa kama familia, tukajadili ikaonekana naweza kukaa peke yangu japo bado nipo chini ya wazazi wangu. Kuhusu vishawishi havinisumbui kwani najitambua.

Ijumaa: Kilichowasukuma mkaamua kupatana na Wema Sepetu ni kipi?

Penny: Sisi ni watu wazima, tuliona haileti picha nzuri kuwa maadui. Sasa hivi tuko na amani na hatutaruhusu watu watugombanishe tena.

Ijumaa: Ni kwa nini unapenda kuvaa nguo fupi?

Penny: Vimini siwezi kuacha ndugu yangu kwa sababu nina mguu mzuri wa kuvaa hivyo, au wewe unanionaje

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI LIKE PAGE YETU HAPO PIA SHARE STORY NA RAFIKI ZAKO
Friday, November 21, 2014



mtoto huyo wa ajabu

My God! Mama aliyetambulika kwa jina la Swaumu Sadick (25), mkazi wa Manzese jijini Dar, amejikuta yeye na manesi wakitimua mbio kwa woga baada ya kujifungua kiumbe wa ajabu.

Swaumu Sadick akiwa hospitali baada ya kujifungua mtoto huyo. Kwa mujibu wa shuhuda wetu, tukio hilo ambalo kwa sasa ni gumzo, lilijiri hivi karibuni mishale ya saa 8:00 usiku kwenye Kituo cha Afya Cha Kijiji cha Mlali kilichopo wilayani Mvomero mkoani Morogoro.

Katika tukio hilo, ilielezwa kwamba Swaumu alijifungua kiumbe huyo wa ajabu anayedaiwa kuwa na mkia mrefu huku akiwa hana miguu. 

Ilidaiwa kwamba baada ya kutokea kwa tukio hilo, baadhi ya ndugu walishikwa na taharuki kubwa huku wengine wakitoa taarifa kwa mwanahabari wetu ambaye alifunga safari kutoka mjini Morogoro na kuwasili kwenye kituo hicho cha afya majira ya saa 12:00 asubuhi. 

Katika mahojiano maalum na mwandishi wa habari hizi  juu ya tukio hilo, nesi wa zamu aliyekutwa kituoni hapo aliyejitambulisha kwa jina moja la Consolatha alikuwa na haya ya kusema:

 “Nilimpokea Swaumu majira ya saa 1:00 usiku akilalamika kuwa na uchungu wa kujifungua. 
Swaumu Sadick akiuguzwa hospitali. “Nilimpa kitanda. Saa 8:00 usiku, uchungu ulizidi nikampeleka leba ambako alijifungua kiumbe huyo mwenye jinsi ya kiume.

 “Baada ya kujifungua na kumuona kiumbe huyu wa ajabu, nilitimua mbio usiku huo kwa woga na kwenda kuamsha manesi wenzangu wanoishi kota za kituo hiki cha afya.
“Nimefanya kazi hii ya ukunga na kuzalisha wazazi zaidi ya 50 lakini sijawahi kukutana na tukio kama hili.”

Kwa upande wake mganga mkuu wa kituo hicho aliyejitambulisha kwa jina moja la Dk. Beatrice alikuwa na haya ya kusema juu ya tukio hilo la kusikitisha: 

“Kimsingi si kiumbe ila ni mtoto ambaye awali tulipomcheki mzazi tulibaini ana kichwa kikubwa na alishafia tumboni zaidi ya siku tatu.“Amezaliwa akiwa na miezi nane tumboni. Tulichokifanya ni kuokoa maisha ya mama jambo ambalo tumefanikiwa.”

 Akizungumza kwa tabu na mwanahabari wetu, Swaumu alisema: “Hii ni mimba yangu ya tatu, ya kwanza iliharibika tumboni, ya pili nilifanikiwa kuzaa salama mwanangu Maimuna.

“Hii ya tatu ndiyo nimejifungua kitu hiki cha ajabu.” 

Alipoulizwa kwa nini aliondoka Dar ambako ndiko kwenye hospitali kubwa na kwenda kujifungulia kijijini akijua ana matatizo ya uzazi, mama huyo alisema:

“Siku za kujifungua zilipokaribia mume wangu Abdallah aliniambia nije kujifungulia kwa bibi yangu Halima, kwa bahati mbaya ndiyo yametokea haya.” 

Kwa upande wake shangazi wa Swaumu aliyekutwa akimhudumia alisema

: “Yameshatokea ya kutokea, tunamshukuru Mungu na tunajiandaa kumchukua mjukuu wetu tukamzike.”
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI LIKE PAGE YETU HAPO PIA SHARE STORY NA RAFIKI ZAKO
Thursday, November 20, 2014


Dakika chache baada ya kuondoka Bongo na kukwaa pipa, bebi mpya wa Diamond, Zari 'The Boss Lady' akiwa ndani ya ndege alionekana mwenye mawazo mazito katika picha alizotupia juzi kwenye fan page yake ya Face Book na Instagram ikisindikizwa na maneno: " miss you already TZ.....deep Mawazu....". Imedaiwa na wadau alikuwa anaamanisha kumkumbuka 'Sukari ya Warembo' zaidi kuliko TZ.....!

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI LIKE PAGE YETU HAPO PIA SHARE STORY NA RAFIKI ZAKO
Sunday, November 16, 2014


Hali Sio Nzuri Ndani ya Bongo Movie! Safari hii yamewakumba mastaa wakubwa klabuni hapo, Devotha Mbaga, Aunt Ezekiel na Jennifer Kyaka ‘Odama’ ambao wanadaiwa kutimuliwa kundini kwa sababu ya kujiweka karibu na mwenyekiti wa klabu hiyo aliyejiuzulu, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’.
Mwanadada anaye tamba katika tasnia ya filamu bongo, Aunt Ezekiel

Kwa mujibu wa chanzo makini kilichozama katika kikao kilichofanyika juzikati, uongozi ambao ulibaki madarakani kundini baada ya Steve kujiuzulu, ulifanya tathmini upya ya memba waliobaki kisha kuwachuja hadi kubaki na wasanii 20 pekee wenye sifa.
“Wamewaengua baadhi ya wasanii ambao wameona hawana sifa ya kubaki kundini, miongoni mwao ni Devotha, Aunt na Odama. Wamesema wanahitaji mastaa wenye msimamo siyo kujipendekeza upande wa Steve, siku si nyingi watayaanika majina ya wenye sifa za kubaki kundini,” kilisema chanzo hicho.
Staa wa filamu bongo Devota Mbaga.

Chanzo hicho kilizidi kumwaga ‘ubuyu’ kuwa, wasanii walioenguliwa ni wanachama hai lakini si wanachama wenye msimamo na baadhi yao wameonesha udhaifu wa kuwa karibu na Steve Nyerere ambaye sasa anafanya harakati zake peke yake.
Baada ya habari hizo kutua katika rada ya Ijumaa, mapaparazi wetu waliwaendea hewani mastaa hao wakubwa waliodaiwa kufukuzwa, mambo yalikuwa hivi:
Mkali wa filamu Bongo, Jennifer Kyaka 'Odama'.

Devotha: Mimi ndiyo kwanza nakusikia wewe siku zote nipo nyumbani sijui hata habari za kikao hicho na sielewi wameniengua vipi wakati mimi ni mwanachama hai na ni miongoni mwa waanzilishi toka tulipokuwa watu saba, lakini kama wameamua hivyo sawa kwani siyo kwamba ukitoka ndiyo mwisho wa maisha.
Odama: Hakuna kitu kama hicho, wanaoenguliwa ni viongozi siyo wanachama, watanienguaje bila kunipa taarifa? Kwanza ndiyo nasikia sijui chochote ndiyo napata taarifa kutoka kwako.

Kwa upande wa Aunt Ezekiel, simu yake iliita bila kupokelewa.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI LIKE PAGE YETU HAPO PIA SHARE STORY NA RAFIKI ZAKO
Saturday, November 15, 2014

BURUDANI

 
Top