Matunda ya asili ni tiba asilia. Pia mchanganyiko wa matunda haya asilia huweza kutengeneza juice tamu ambayo pia huweza kuwa tiba asilia.
Zifuatazo ni baadhi ya Juice ambazo unaweza tengeneza wewe mwenyewe hapo nyumbani na zikawa ni kama tiba kwako;
TUFAHA NA TANGO LA KAWAIDA
Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya huondoa harufu mbaya mdomoni na hupunguza joto la mwili.
CHUNGWA, TANGAWIZI NA TANGO
Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya hung’arisha rangi ya ngozi na kuifanya kuwa laini. Pia hupunguza joto la mwili. Kwa wale wenye matatizo ya kuwa na ngozi kavu, juisi hii itawasaidia sana.
NANASI, APPLE NA TIKITIMAJI
Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya hufanya kazi ya kuondoa chumvi nyingi mwilini, husafisha kibofu cha mkojo na figo. Juisi hii ni nzuri kwa wale wenye matatizo ya kibofu na figo au wanaotaka kujikinga na magonjwa hayo.
APPLE, TANGO NA ‘KIWI’
Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya hung’arisha rangi ya ngozi. Kiwi ni aina ya matunda ambayo hujulikana pia kama ‘matunda-damu’.
PEASI NA NDIZI
Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya hurekebisha kiwango cha sukari katika damu. Inawafaa sana wagonjwa wa kisukari na inaweza kuwa sawa na kinga dhidi ya ugonjwa huo.
KAROTI, PEASI, APPLE NA EMBE
Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya huzuia athari ya sumu mwilini, hupunguza shinikizo la damu na kuondoa mlundikano wa uchafu mwilini. TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment