Je huu ni ukweli kwamba hakuna njia ya mkato kuelekea mafanikio? Inawezekana
unasema ‘Awali hujui mambo yanayoendelea na utabakia hivyo hivyo’. Kuna
kitu nimeendelea kujifunza kwa watu matajiri wanaochipukia kwenye
Forbes magazine na kwingineko.
Siku
chache zilizopita katika Kongamano fulani ambako Mjasiriamali wa Kenya
Julian Kyula na Heshan De Silva waliongea kutokana na uzoefu na historia
ya Maisha yao. Kitu kimoja cha kufanana ni kutumia kile ulichonacho na
uweze kukiendeleza kufikia kule unakotaka.
Hakuna Njia ya Mkato kwenye Mafanikio; Kama
kuna kitu ambacho hatutaweza kuendelea ni kupitia njia za mkato. Njia
za mkato haziwezi kujenga maendeleo yako wala hutoweza kuacha kitu
kiuchumi. Kwanini? Kuwa na fedha ambayo huna maelezo nayo au
haujaiwekeza kwenye njia sahihi ni kupoteza hiyo mali.
Mimi
huangalia zaidi upande chanya zaidi kuliko upande hasi, kwa kila mtu
ambaye namtolea mfano naangalia upande chanya, kama una kitu hasi juu ya
yeyote huo sio upande wangu wa makala hii.
Kuna
njia nyingi za utafutaji wa mafanikio “kama kupanda na kuvuna” kitu
ambacho watu wengi wanapenda, vilevile biashara za njia ya mitandao ili
upate kamisheni kwaajili ya watu wanaojiunga chini yako. Hizo hazijawahi
kuwa njia sahihi za kufanikiwa mara nyingi zinaishia kutapeliwa.
Kufanya kazi kwa umakini na sio kwa nguvu. Umakini
unaozungumziwa hapa ni kuwa na watu sahihi au mtandao sahihi wa watu
kuhusu biashara au bidhaa unayoifanya. Umakini huo utakusaidia kufikia
malengo yako, haimaanishi kwamba hautakutana na vikwazo mbalimbali ila
je una umakini gani kupambana na vikwazo hivyo?
Inabidi Ukuze kitu ulichonacho. Watu
wengi tunaogopa kuchukua hatua ya kuamini kwamba kitu ulichonacho
kinaweza kuwa kitu kikubwa cha kuweza kukutengenezea ajira yako na watu
wengine. Tunakuwa na sababu nyingi na za kutosha kuonyesha kwamba
haiwezekani. Ila ukweli uko hivi kwako haiwezekani ila kuna mtu sehemu
fulani usiyoijua wewe kimewezekana. Hivyo inategemea mtazamo wako ukoje.
Vitu vingi tunavyovifanya sasa hivi wazee wetu hawajawahi kufikiri
kwamba vitawezekana lakini vinafanyika na wanaona vinawezekana, hivyo
badilisha unavyofikiri unaweza ukabadiisha matokeo ya vitu unavyofanya
kila siku. Nuia Kukua kimtizamo na kiutendaji.
Sisi
sote ni matokeo ya maamuzi tunayofanya kila siku kuhusu maisha yetu,
hivyo mwenye maamuzi ni wewe mwenyewe kufanya kilicho sahihi au kuamini
na kufanya kulingana na habari za mtaani.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment