HILI nalo janga! Mwanaume
mmoja anayesemekana ni mfanyabiashara ambaye pia anatajwa kugombea
udiwani wa kata moja iliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam, aliyetajwa
kwa jina moja la mzee Beno amenaswa akiwa chumba cha gesti na denti wa
chuo kimoja kilichopo Kibamba jijini Dar, Ijumaa ‘kubwa’ lina mkanda
wote.
Mzee Beno akificha sura kwa aibu ili asipigwe picha.
Tukio
hilo la aina yake lilijiri Oktoba 20, mwaka huu ndani ya gesti moja
(jina tunalo) iliyopo Kimara-Suka jijini Dar es Salaam ambako mama mzazi
wa wa binti huyo ndiye aliyemnasa mheshimiwa mtarajiwa huyo na binti
yake.
WASIWASI KWANZA
Awali,
mama huyo alisema alianza kuwa na wasiwasi na mwenendo wa binti yake
huyo kutokana na kuanza kale katabia ka’ kuchelewa mara kwa mara kurudi
nyumbani akitoka chuoni, akajiongeza!
“Sisi tulishajua binti
yetu ameanza katabia kabaya, akienda shuleni anachelewa kurudi wakati si
kawaida yake, tukasema kuna jambo linaendelea kwake,” alisema mzazi
huyo.
...Akidhibitiwa baad ya kufumaniwa.
USHUSHUSHU
Kwa
mujibu wa mzazi huyo aliyeonekana kufura kupita tafsiri ya neno
lenyewe, alianza kibarua cha ushushushu kama si upelelezi wa kumfuatilia
binti yake ambapo siku moja aliifanyia udukuzi simu yake na kukuta
ujumbe mfupi wa maneno (SMS) kwenye simu hiyo ukimtaka afike kwenye
gesti hiyo.
MBALI NA UJUMBE
Ikadaiwa
kuwa, mbali na SMS hizo, mama huyo aliwahi kumsikia binti yake akiwa
hewani na ‘mheshimiwa’ huyo jambo lililozidisha hasira zake kama mama
akiamini kuna mwanaume anamharibu binti yake aliye na malengo naye
mazuri siku za usoni.
Mfanyabiashara na denti huyo wakijutia kwa kitendo walichokifanya.
BINTI ATII AMRI YA WAZAZI
Ndipo mama huyo akamuweka kikao kifupi binti yake na kumtaka aseme ukweli kuhusu mtu aliyemuita gesti Kimara-Suka.
NI KAMA WALISEMA
“Mtu gani mama?”
Mama: “We’ usinitanie, nimekuta meseji kwenye simu yako, kuna mwanaume umemsevu kwa jina la Sweet, amekuita gesti, ni nani?”
Binti: “Aaah! Ni mzee mmoja hivi.”
Mama: “Anaitwa nani?”
Mfanyabiashara huyo akisihi kuachiwa baada ya kufumaniwa.
Binti: “Anaitwa mzee Beno.”
Mama: “Ni mpenzi wako?”
Binti: (moyoni) “mama
bwana, sasa si umeona nimemsevu Sweet anaweza kuwa mjomba ‘angu kweli?
(kwa sauti) “ndiyo mama lakini sijawahi kufanya naye chochote hata siku
moja.”
Mama: “Apia.”
Binti: “Hakyamungu vile.”
MTEGO
Ikadaiwa
kuwa baada ya hapo, binti akatakiwa kumjibu mzee huyo kwamba anakwenda
wakutane huko gesti ili wamalizane kwani ‘amemmisi’ sana siku hiyo,
mzee akashindwa kujiongeza.
Binti akiwa na mzazi wake
na skwadi nyingine walianza safari ya kwenda Kimara –Suka kwenye gesti
hiyo ambapo walikaa baa ya jirani, binti akaenda ndani ambako mzee huyo
alishafika zamani gani na kumsubiri.
Bw. Beno akiwa nje ya gesti hiyo iliyopo kimara suka mara baada ya kufumaniwa.
Baada
ya muda, binti alituma meseji kwa mama yake akisema mambo tayari, wapo
‘weupe pee’ (hawana nguo). Ndipo mama huyo akachukua timu yake na
kuvamia gesti hiyo kwa ajili ya kulianzisha.
OFM YAKATIZA MITAANI, YAKUMBANA NA KASHESHE
Oparesheni
Fichua Maovu ‘OFM’ ya Global Publishers ilikuwa ikikatiza mitaani
kusaka matukio kwani ni ada yake, ndipo walipoibukia eneo lenye gesti
hiyo na kukumbana na kasheshe hilo la nguvu.
“Hawa wazee ndiyo wale
ambao wanaharibu watoto wa watu huku yeye wanawe wakisoma vizuri na
hakuna anaowaharibia masomo yao,” alisikika akichonga mama huyo.
Akaendelea: “Jamani nawaomba njooni na makamera yenu yote hapa.”
OFM YAPATA NGUVU
Kufuatia maneno ya mama, OFM walipata nguvu na kuanza kupiga picha za kumwaga kwa ajili ya kumbukumbu.
MGOMBEA ASEMA NENO
Huku
akiwa amekaa kwa tafakuri ya kina, mzee Beno alisema ameumbuka na
kuitaka familia ya mwanafunzi huyo kumalizana kifamilia nje ya gesti
hiyo huku akiwaomba OFM chondechonde wasiitoe habari gazetini.
Hata hivyo, mpaka tunakwenda mitamboni, mwanamke huyo alisema hawajamalizana chochote hivyo OFM inaendelea kufuatilia sakata hilo.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment