Bi Cheka akiwa nje ya nyumba
anayoishi.
DAH MASIKINI! Hivi ndivyo unavyoweza
kusema wakati unapomuona msanii wa
muziki wa kizazi kipya, Cheka Hija,
maarufu kama Bi. Cheka kutoka Kundi la
Mkubwa na Wanawe, linaloongozwa na
Said Fella ‘Mkubwa’ lenye maskani yake,
Temeke jijini Dar es Salaam.
Mtoa habari wetu aliwasiliana na gazeti hili
na kulieleza kuwa msanii huyo mwenye
umri wa miaka 55, hivi karibuni alianguka
ghafla nyumbani kwake na kukata kauli,
wakati alipokuwa akienda chooni
kujisaidia.
Wikiendi iliyopita, Amani lilifika nyumbani
kwa msanii huyo mzee, anayeishi Bunju B,
nje kidogo ya jiji la Dar na kumkuta akiwa
na wajukuu zake huku hali yake ikiwa tete
tokea alipoanguka Oktoba mwaka huu .
Akiwa anaishi katika kijumba chake
kilichojengwa kwa miti na kukandikwa
udongo, mtu anayemuona katika luninga
akifanya vitu vyake, asingeweza kuamini
kama hapo ndipo anapoishi.
Upande wa nyumba yake.
“Ukweli nilikuwa na hali mbaya, afadhali
sasa, naongea na kusimama kwani nilikuwa
siwezi kutembea, wiki iliyopita alikuja
meneja wetu, Yusuf Chambuso na akina
Dogo Aslay.
“Jamani maisha yangu kwa sasa ni magumu
kwani siwezi kufanya kazi yoyote na sina
msaada na kwenye muziki sijaona faida
yoyote labda ya nguo tu, kwamba nilizoea
kuvaa madela na kanzu sasa nina suruali,”
alisema Bi Cheka kwa machungu.
Bi Cheka akiwa na wajukuu zake.
Alisema anasikitishwa na maisha yake
kwani kutokana na umaarufu wake, mtaani
kwao anaonekana kama mtu mwenye
uwezo, wakati siyo kweli kwani anaishi
kwenye nyumba ya tembe katikati ya
nyumba nzuri.
“Kuhusu malipo makubwa kuwahi kupata
ni shilingi laki tatu nilizolipwa kwenye shoo
ya Fiesta mwaka juzi, hizo ndizo hela
kubwa niliyowahi kupata katika
muziki.”Gazeti hili lilimtafuta Fella ambaye
alikiri Bi. Cheka kuumwa, akisema
anasumbuliwa na magonjwa ya uzee na
kwamba ahadi yake ya kumsaidia kujenga
nyumba imeishia kwenye mchango wake
wa matofari.
...Bi Cheka akiimba na Chege.
“Mimi kama Fella nimesaidia ninapoweza,
nimemchangia matofari kidogo, kwa hiyo
watanzania wenzangu nao tuungane
tumchangie ili aweze kurekebisha kibanda
chake,” alisem
Global Publishers inaanzisha kampeni
maalum ya kumsaidia na hivyo inawaomba
watanzania kumchangia msanii huyu ili
apate nyumba nzuri na matibabu yake. Ili
kumsaidia tuma fedha kwenye namba
0654-880707 ambayo itasimamiwa na
kampuni.
Related Posts
MASHABIKI WAMCHARUKIA ALI KIBA, NA KUMPA MAKAVU LIVE BAADA YA KUACHIA VIDEO YA MWAKA ISIYOENDANA NA MAZINGIRA ..SOMA UJUE WALICHOSEMA
Laty Side video haiendani na alichoimba yan nikupiga wimbo wa taifa disco Fad Marlon Fad Mbay hyo ja[...]
Wema Sepetu Amfuata Diamond Platnumz Kampala Uganda...Je Wawili Hawa Wanafuatana au Wanarushana Roho? Usiku wa juzi tarehe 18, jiji la Kampala nchini Uganda lilipambwa na “EVENTS” mbili mkubwa kwenye upande wa buruani ambazo ni Show kubwa ya mwnamziki Jose Chameleone iliyofahamika kama 1Man Show Million na Pati ya mwanamama Zari iliyofahamika kama Zari All White Ciroc Party. Mwigizaji Wema Sepetu na mwanamziki Diamond Platnumuz wote walitua nchi humo na kugawana matukio hayo kama ifuatavyo; Wema Sepetu ambae anadai ni amekuwa shabiki mkubwa wa masanii Jose Chameleone alitokea nchini Ghana na kutua jijini Kampala kuhudhuria show ya mwanana mziku huyo ambayo ilifanyika Serena Hotel. Wakati Diamond Platnumz ambae kwasasa ana “Le Project” na mwanamama Zari alihudhulia pati ya Zari kama “Special Guest”. Baadhi ya watu wamechukulia kitendo hiki ni kama mwanadada Wema “Amepaniki” hivi, Huku wengine wakisema kuwa Wema ana uhuru wakufanya kile anachokitaka bila ya kuhofia watu watasemaje. Jambo hili halijatokea kwa bahati mbaya kwani wiki kadhaa zilizopita, Diamond alipoonyesha kum- support Zari kwenye pati yake,Wema nae alibuka na kum-support Jose. Kama unavyoona hapa chini. Maoni yako tafadhari, Je wawili hawa wanatafutana au wana rohorushana
Usiku wa juzi tarehe 18, jiji la Kampala nchini Uganda lilipambwa na “EVENTS” mbili mkub[...]
DIAMOND AONGE HAYA Wema, Jokate, Penny Hawakutaka Kuzaa Na Mimi
DIAMOND:Wema, Jokate, Penny Hawakutaka Kuzaa Na Mimi Akizungumza kwenye kipindi cha Live Ch[...]
Muimbaji wa Nyimbo za INJILI Tanzania Florah Mbasha Aomba Talaka Mahakamani K
kazi kisutu, akiomba kuvunja ndoa kati yake na mumewe, Emmanuel Mbasha. Flora anadai sababu za kuomb[...]
Staa huyu wa Nollywood aeleza sababu za kwa nini hayupo tayari kuingia katika maisha ya ndoa kwa sasa
Mwigizaji wa Nollywood Genevieve Nnaji amefunguka kuhusu hatma ya maisha yake ya ndoa na kueleze[...]
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.