Mara
baada ya kupata ushimdi wa jumla ya 3-1 dhidi ya timu ya taifa ya
Slovenia kwenye uwanja wa Wembley hapo jana washabiki wa timu ya Taifa
ya Uingereza wamempachika jina la "Wele" wakimfananisha na gwiji la soka
la nchini Brazil Pele.

Wengine
wamekwenda mbali zaidi kwa kumfananisha mchezaji huyo na mtoto wa
familia ya kifalme kutokana na raha waliyopewa na mchezaji huyo mara baada ya kuifungia timu hiyo ya taifa jumla ya magoli mawili.
Mashabiki
wa timu ya taifa ya Uingereza wanaonekana kujikuta wakiingia kwenye
furaha iliyopitiliza kutokana na ari inayooneshwa na timu yao hiyo kwani
mara ya mwisho timu hiyo iliwahuzunisha sana mashabiki wake kwenye
michuano ya kombe la Dunia walipotolewa kwenye hatua za awali za
michuano hiyo dhidi ya timu ya taifa ya Italia.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment