Mapenzi bhana! Baada ya kutoka
kimalavu na kumwagana na mwanadada
mwenye mvuto Bongo, Wema Isaac Sepetu
‘Beautiful Onyinye’ kisha kuangukia
kwenye ‘utamu’ wa penzi la mwanamama
anayekimbiza Uganda, Zarinah Hassan
a.k.a Zari au The Boss Lady, Nasibu Abdul
‘Diamond Platnumz’ ameamua kuanika siri
tano za kilichomvutia kwa staa huyo
gumzo Afrika Mashariki.
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’
akiwa na mwanamama anayekimbiza
Uganda, Zarinah Hassan a.k.a Zari au
The Boss Lady.
Akizungumza katika mahojiano maalum
katika ofisi za gazeti hili, Bamaga-Mwenge
jijini Dar hivi karibuni, bila kupepesa
macho au kuuma maneno baada ya
kuulizwa kinagaubaga juu ya ukaribu wake
na Zari, Diamond au Dangote hakutaka
kuficha, akaamua kuweka mambo yote
hadharani.
MATANGAZO
Alifunguka: “Mimi ni mwanamuziki
mkubwa na mwenye heshima, wakati
mwingine natakiwa kuwa na akili ya kuwa
na uhusiano na watu ambao watakuwa
msaada kwangu pia.
“Siwezi kuwa karibu na mtu ambaye
hataniongezea kitu chochote kile. Baada ya
kujitangaza sana Tanzania, nikahamia
Kenya ambapo nilikuwa karibu na
mwanadada Avril. Ukaribu wangu kwake,
ukanifanya Kenya kutambulika.
“Baada ya kukaa kwa muda, nikataka
nitambulike na Uganda pia, unafikiri
ningefanya nini? Nikaliteka soko lao kwa
kuwa karibu na mrembo Zari.
“Kweli nimefanikiwa na hata siku ya shoo
yake (Desemba 18, mwaka huu nchini
Uganda), ilikuwa ni balaa kiasi kwamba
sikuamini kilichokuwa kimetokea, watu
walikuwa nyomi ile mbaya. Mbali na kuwa
mwanamuziki mkubwa, bado nahitaji
kujitangaza zaidi.”
Zari na Diamondi wakibusiana
kimahaba.
MSISIMKO
Sababu ya pili aliyoitaja ni kwamba Zari
ambaye ni mama wa watoto watatu ana
msisimko wa aina yake tofauti na ‘mashori’
wengine aliwaowahi kuanguka nao
dhambini.
“Hakuna mwanaume anayependa kukaa na
msichana asiyekuwa na msisimko wa
kimapenzi. Hebu fikiria umekaa na
mwanamke mwenye umbo kama la
mwanaume, utapata msisimko gani hapo?
Lakini mcheki mtoto alivyong’aa,
anameremeta, mtoto yupo bomba, ukikaa
karibu yake tu utagundua kwamba umekaa
na msichana mwenye mvuto ambaye kila
wakati atakufanya kuwa bize
kumwangalia.”
BIASHARA
Sababu ya tatu aliyoitaja Diamond ni
kwamba mwanadada huyo yupo vizuri
kibiashara.
“Ninaangalia fedha, ili biashara zangu
ziweze kupiga hatua sina budi kukaa
karibu na mfanyabiashara mwenzangu
(Zari) kwa ajili ya kushauriana biashara
ziende vipi.
“Yeye (Zari) ni mkongwe katika biashara,
kuwa karibu naye naamini nitajifunza
mambo mengi sana.
Amekuwa muwazi kwangu na amenipa
mianya mingi ya kufanya biashara, lakini je,
nisingekuwa karibu naye, michongo hiyo
ningeipata vipi?”
Zari na Diamondi wakiwa kwenye pozi.
UZURI
Sababu ya nne ya kuwa na Zari, Diamond
alidai kwamba mwanamama huyo ni mzuri
kupita maelezo.
Alifunguka: “Mimi ni mwanamuziki
mkubwa, watoto wazuri wananipenda kwa
hiyo kama ningefanya uamuzi wa kuwa na
mwanamke asiyekuwa mzuri, maneno
yangeanza kusikikasikika na isingekuwa
poa. Mbali na kuwa mfanyabiashara,
kumtumia kama msaada wa kunitangaza,
lakini Zari ni mzuri bwana. Ni mwanamke
ambaye kwa kumwangalia tu, unaweza
kusema kwamba haujawahi kukutana na
mwanamke mzuri kama yeye.
ANAJITAMBUA
Sababu ya mwisho aliyoianika Diamond ni
kwamba Zari yupo vizuri kichwani kwa
maana ya kujitambua tofauti na wanawake
wote aliowahi kutembea nao.
Mwanadada mwenye mvuto Bongo,
Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’.
“Nimekuwa na wanawake tofautitofauti
lakini kwa Zari, ni mwanamke mwenye
hekima na anajitambua sana. Si
mzungumzaji kivile na huwa anapenda
kufanya vitendo kuliko maneno.
“Anajua ni kipi anatakiwa kufanya na akili
yake ameielekezea kwenye fedha zaidi.
Hapendi masihara na fedha, anapenda
kujitoa na ni mchakarikaji sana. Nampenda
mwanamke wa hivyo kwa kuamini
kwamba atanifanya nijitume zaidi.”
AWACHAMBUA JOKATE, WEMA NA
PENNY
Diamond alipoulizwa juu ya kasoro za
warembo wakali Bongo aliowahi kutoka
nao wakiwemo mrembo Jokate Mwegelo
‘Kidoti’, Wema na mtangazaji wa Radio E-
FM, Penniel Mungilwa ‘Penny’,
aliwachambua mmoja baada ya mwingine
na kuhitimisha kuwa ni wazuri lakini
hawamfikii Zari.
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
UTAMBULISHO KESHO DAR LIVE
Mbali na kuziweka wazi sifa za Zari, jamaa
huyo alidai kwamba atamtambulisha rasmi
kwa Wabongo kesho usiku kwenye Uwanja
wa Kimataifa wa Burudani wa Dar Live,
Mbagala jijini Dar atakapokuwa
anaangusha burudani ya kibabe katika
Tamasha la Wafalme akiwa na mfalme
mwenzake, Mzee Yusuf na wakali wengine
kibao kwa kiingilio cha shilingi 10,000/=
kwa kawaida na shilingi 20,000/= kwa
V.I.P.
Home
»
UDAKU
» MAPENZI BHANA! DIAMOND
AANIKA SABABU 5 ZA
KUMPENDA ZARI!
KUMTAMBULISHA X-MASS,
AWACHAMBUA MA-EX WAKE!
Related Posts
Wema Sepetu Amfuata Diamond Platnumz Kampala Uganda...Je Wawili Hawa Wanafuatana au Wanarushana Roho? Usiku wa juzi tarehe 18, jiji la Kampala nchini Uganda lilipambwa na “EVENTS” mbili mkubwa kwenye upande wa buruani ambazo ni Show kubwa ya mwnamziki Jose Chameleone iliyofahamika kama 1Man Show Million na Pati ya mwanamama Zari iliyofahamika kama Zari All White Ciroc Party. Mwigizaji Wema Sepetu na mwanamziki Diamond Platnumuz wote walitua nchi humo na kugawana matukio hayo kama ifuatavyo; Wema Sepetu ambae anadai ni amekuwa shabiki mkubwa wa masanii Jose Chameleone alitokea nchini Ghana na kutua jijini Kampala kuhudhuria show ya mwanana mziku huyo ambayo ilifanyika Serena Hotel. Wakati Diamond Platnumz ambae kwasasa ana “Le Project” na mwanamama Zari alihudhulia pati ya Zari kama “Special Guest”. Baadhi ya watu wamechukulia kitendo hiki ni kama mwanadada Wema “Amepaniki” hivi, Huku wengine wakisema kuwa Wema ana uhuru wakufanya kile anachokitaka bila ya kuhofia watu watasemaje. Jambo hili halijatokea kwa bahati mbaya kwani wiki kadhaa zilizopita, Diamond alipoonyesha kum- support Zari kwenye pati yake,Wema nae alibuka na kum-support Jose. Kama unavyoona hapa chini. Maoni yako tafadhari, Je wawili hawa wanatafutana au wana rohorushana
Usiku wa juzi tarehe 18, jiji la Kampala nchini Uganda lilipambwa na “EVENTS” mbili mkub[...]
Staa huyu wa Nollywood aeleza sababu za kwa nini hayupo tayari kuingia katika maisha ya ndoa kwa sasa
Mwigizaji wa Nollywood Genevieve Nnaji amefunguka kuhusu hatma ya maisha yake ya ndoa na kueleze[...]
AT ASHINDA KESI DHIDI YA MGANGA WA JADI ALIYEMSHITAKI KWA KUTOMLIPA PESA BAADA YA KUPANDISHA NYOTA YAKE
Muimbaji wa Mduara, AT ameshinda kesi iliyokuwa ikimkabili nailiyofunguliwa na mganga wa jadi k[...]
PICHAZ: UNAAMBIWA HUYU NDIYE MBUNGE MZURI KULIKO WOTE NCHINI KENYA
Anajulikana kwa jina la Naisula Lesuuda ambaye aliwahi kuwa mwandishi wa kituo cha Tv kenya cha KBC [...]
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.