Wananchi mkoani kagera wamepinga
uamuzi wa Rais wa jamuhuri ya muungano
wa Tanzania Dk Jakaya Mrisho Kikwete
kwa kumuondoa madarakani waziri wa
ardhi nyumba na makazi na kuwaweka
kiporo viongozi wengine walioshiri
kuhujumu pesa za akaunti ya Tegeta
Escrow.
Wakiongea na ITV wananchi wa mkoa huo
wamesema hawajajua nini hatima ya Rais
wa jamuhuri ya muungano wa tanzania Dk.
Kikwete kwa kuwaweka Kiporo mawaziri
wengine waliohusika katika sakata hilo na
kumuuondoa waziri Tibaijuka napia
wamebaki na sintofahamu ambapo
wamemtaka Rais kutoa ufafanuzi kuwa
licha kumg’oa madarakani kiongozi huyo
Je, Pesa hizo zitarudishwa kwenye akauti
hiyo ya TEGETA ESCROW au la.
Nao baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa
vya mkoa huo akiwemo katibu wa siasa na
uenezi wa chama cha mapinduzi mkoa wa
kagera Hamimu Mahamudu amepongeza
uamuzi wa Rais alioutoa jana wakati
akiongea na wazee wa jijini Dar es salaam
kwa kumuondoa kiongozi huyo huku
katibu wa chama cha Demokrasia na
maendeleo chadema katika manispaa ya
Bukoba Victor Sherejei akisema kuwa Rais
hajatoa uamuzi sahii ambapo amemtaka
Rais kuwafahamisha watanzinia kuwa Pesa
za Escrow zitarudishwa lini katika akanti
hiyo au kuwaondoa viongozi hao
madarakani ndio suluhisho la kwamba pesa
hizo hazirudishi?
Kwa upande wake aliyekuwa Waziri wa
ardhi nyumba na makazi Profesa Anna
Tibaijuka amesema licha Rais kumuondo
katika nafasi yake aliyokuwa nayo sasa
amerudi jimboni kwake kwa ajili ya
kutatua kero na changamoto mbalimbali za
wananchi wake kwani nafasi
aliyokuwanayo ilikuwa haimpi nafasi ya
kuwasimamia wananchi katika jimbo lake
na kwamba pesa hizo alipewa na
Lugemalila zilikuwa za kusaidia shule na
alipewa kama zawadi bila kujua kama pesa
hizo zilitoka katika akaunti ya TEGETA
SCROW ndio maana hakutaka kujiuzulu
mapema.
Related Posts
Breaknewz msanii diamond aamuwa kugombea ubunge mwaka2015
Mwanamuziki wa kizazi kipya diamond ameandika katika ukurasa wake wa facebook kuwa ameamua hay[...]
LOWASA: SAKATA LA RICHMOND HAKUNA ALIYESIMAMA NA KUNITETEA, LEO HII WANATETEA WIZI WAZI WAZI
Haya ndio Maneno aliyoyasema Lowassa Kupitia Account yake ya Twitter kuhusu Sakata la Wizi wa Pe[...]
BREAKING NEWZ:KURA ZACHOMWA MBELE YA MAKADA WA VYAMA VYA SIASA
Zoezi la kuchoma kura zilizopigwa katika kituo cha twiga likiendelea katika ofisi [...]
HII NDO NYUMBA INAYO MILIKIWA NA KIGOGO WA ESCROW…CHEZEA PESA WEWE
HUKU moto wa upotevu wa fedha za umma katika akaunti ya Tegeta Escrow ukiwa bado unawaka kufuat[...]
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.