MCHEPUKO?
STAA wa kitambo kwenye tasnia ya filamu za Kibongo, Stanley Msungu
amenaswa laivu akiwa kwenye pozi tata na mke wa mtu aliyetambulika kwa
jina moja la Bonita.
Tukio hilo lilijiri nje ya Mgahawa wa Great Wall uliopo Masaki jijini
Dar, usiku wa saa saba ambapo kulikuwa na tafrija ya chakula cha usiku
iliyoandaliwa na Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve
Nyerere’.
“Dah! Kuna watu wana uhuru kweli na ndoa zao, yaani Bonita amefunga ndoa
juzijuzi tu, mumewe amelala nyumbani yeye anahangaika huku na Msungu.
“Kama huamini nenda kwenye gari ukajionee wanachofanya Msungu na Bonita
au hadi tufanye sisi ndiyo mnatupiga picha?” alihoji mmoja wa waigizaji
walioalikwa kwenye hafla hiyo ambaye jina tunalihifadhi akimsisitiza
mwanahabari wetu kwenda kunasa tukio hilo.
Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, Risasi Jumamosi kama kawaida yake
lilinyata hadi lilipokuwa gari la Msungu kisha kunasa tukio hilo ambapo
Bonita alikuwa akijificha asionekane vizuri huku Msungu akiwa katika
hali ya kutaharuki.
“Kaka mke wa mtu huyu, utaniharibia mimi na yeye kwa mumewe, achana na
hayo mambo kaka njoo tuzungumze,” alisema Msungu akijitetea huku Bonita
akiomba kamera ya paparazi wetu iishe chaji ili zoezi la kupiga picha
lisiendelee kabla ya kuondoka eneo hilo kwa spidi na kutaka kumgonga
mwandishi.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.