Uchaguzi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA,wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga umeingia dosari,baada ya mmoja wa madiwani wa chama hicho kuhusishwa na rushwa na vitendo vya usaliti ndani ya chama kutoka CCM.
Pia
katika uchaguzi huo baadhi ya wagombea wamechapana makonde baada ya
kuenguliwa kwa baadhi ya majina ya wagombea katika uchaguzi wa Baraza
la Vijana wa chama hicho (BAVICHA),huku Red Brigade wakihusika katika
vurugu hizo.
Hali
hiyo ilitokea juzi mjini Kahama katika ukumbi wa Mamba Hall, baada
mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Chama hicho wilayani Kahama Leonard
Mayala ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Nyasubi, alienguliwa kuwania
nafasi hiyo baada ya kubainika kutumia rushwa kuomba achaguliwe katika
nafasi hiyo.
Mgombea
huyo alituhumiwa kutumia shilingi milioni mbili kuwahonga baadhi ya
wanachama,fedha ambazo zinadaiwa zilitolewa na baadhi ya makada wa Chama
cha Mapinduzi kwa njia ya mtandao wa (Mpesa)ili kuhakisha ananyakuwa
nafasi hiyo.
Tuhuma
hizo zimekuja baada ya wanachama kutokuwa na imani naye kutokana na
mwenendo wa diwani huyo wa kuwa karibu na makada wa CCM wilayani hapa na
hivyo kusababisha viongozi na wasimamizi wa uchaguzi huo kuengua jina
lake baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na kuwekewa pingamizi.
Aidha
katika uchaguzi huo baadhi ya wagombea na wanachama walichapana makonde
wakipinga kuenguliwa majina ya baadhi majina ya wagombea katika
uchaguzi wa Baraza la Vijana wa Chadema (BAVICHA).
Ugomvi
huo ulitokea baada ya wagombea waliopitishwa katika nafasi ya
Uenyekiti wa Bavicha kuanza kujinadi kwa wananchama ndipo mgombea
Thomas Masanja aliyeenguliwa katika kinyang’anyiro hicho kutokana na
kukosa sifa ikiwemo kadi yake ya uanachana kutotambulika alijitokeza na
kuzuia uchaguzi.
Kufuatia
kuenguliwa kwa mgombea huyo ndipo badhi ya wafuasi wake wakiwemo Red
Brigade walipojitokeza na kuanza kufanya fujo kwa lengo la kuzuia
uchaguzi huo kuendelea wakidai kwamba mgombea wao kutotendewa haki kwa
kuenguliwa kinyemela kugombea nafasi hiyo.
Hali
hiyo ilikwenda mbali zaidi kwani wafuasi hao walianza kuwashambulia
baadhi ya viongozi na wasimamizi ambapo Mwenyekiti wa Chadema wa
Halmashauri ya Msalala Emmanuel Bombeda alipigwa ngumi na Red brigade
waliokuwa wakimuunga mkono mgombea aliyeenguliwa.
Utulivu
na amani urejea ukumbini humo baada ya msimamizi wa uchaguzi wa Chama
hicho kanda ya Ziwa Mashairiki,Madata Sande kuingilia kati na kuwataka
wanachama kuwa wavumilivu ili kufanikisha uchaguzi huo kwani wagombea
walioenguliewa katika kinyang’anyiro hicho walienguliwa kihalali bila
upendeleo wowote kwa kuzingatia katiba ya chama hicho.
Katika
uchaguzi huo wajumbe walimchagua Juma Protas,kuwa Mwenyekiti wa
Chadema wa wilaya hiyo,naye Mshibu Peter akiteuliwa kushika nafasi ya
Ukatibu wa chama hicho,nafasi ya Ukatibu Uenezi ikimwangukia Anord Peter
na Mweka Hazina alichaguliwa,Elias Mayunga.
Nalo
Baraza la Vijana BAVICHA lilimchagua Samwel Peter kuwa Mwenyekiti wake
na ndani ya uchaguzi huo wajumbe walichagua viongozi mbali mbali wa
yakiwemo mabaraza ya Wazee,Wanawanake na wajumbe wa mkutano mkuu taifa
wa chama hicho.
0 comments:
Post a Comment