Sakata la umri la
Miss Tanzania 2014 Sitti Mtevu limeendelea kuchukua sura mpya baada ya
Baraza la Sanaa Taifa (Basata) kudai kuwa litamvua taji hilo endapo
watagungua kasoro za umri zinazodaiwa.
Akizungumza na gazeti la Nipashe, Katibu Mkuu wa Basata, Geoffrey
Mwingereza , alisema wanasubiri uchunguzi wao ukamilike na wakibaidi
udanganyifu watamvua taji hilo. Wakati Mwingereza akielezea taarifa
hiyo, viongozi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
wanatarajia kukutana leo jijini Dar es salaam kwajili ya kujadili sakata
hilo.
Akizungumza na gazeti hilo jana, Naibu Waziri wa Wizara ya Michezo, Juma
Mkamia alisema serikali imelisikia sakata la mrembo huyo na wamamua
kuitisha kikao ili kulifanyia kazi. “Siwezi kukuambia hatua gani
zitachuliwa, ila kesho, (leo) tutakuwa na kikao , serekali haiwezi kukaa
kimya , kuna vyombo vyake vinalifanyia kazi,” alisema Mkamia.
Aliongeza kuwa yeye alikuwa nje ya Dar es Salaam lakini kuna maelezo aliyoyatoa na yameanza kufanyiwa kazi.
0 comments:
Post a Comment