Kushoto ni mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Shinyanga(SHIREFA) Benesta Rugora akitoa taarifa kwa waandishi wa habari mjini Shinyanga leo kuhusu  mchezo wa ligi kuu ya Vodacom 2014/2015 kati ya Stand United na Young Africans utakaochezwa siku ya Jumamosi wiki hii katika uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga.Kulia kwake ni katibu wa SHIREFA Mwalimu Said Nassoro

Kushoto ni mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Shinyanga(SHIREFA) Benesta Rugora,kulia kwake ni ni katibu wa SHIREFA Mwalimu Said Nassoro.
Maandalizi ya mchezo wa ligi kuu ya Vodacom 2014/2015 kati ya Stand United na Young Africans utakaochezwa siku ya Jumamosi wiki hii katika uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga yamekamilika.

Akitoa taarifa leo kwa waandishi wa habari mjini Shinyanga mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Shinyanga(SHIREFA) Benesta Rugora amesema mchezo huo utachezwa siku ya Jumamosi Oktoba 25,2014 saa  kumi jioni katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.

Amesema tiketi zitauzwa siku ya mchezo kuanzia saa mbili asubuhi ambapo kiingilio ni shilingi elfu kumi jukwaa kuu na elfu tano mzunguko na tiketi hazitauzwa uwanjani.

"Kutakuwa na vituo 10 katika manispaa ya Shinyanga vya kuuza tiketi,kituo cha kwanza kitakuwa kwenye bwalo la Jeshi la polisi nje ya uwanja wa Kambarage,vingine ni Bwalo la polisi,Rubafu-Rwegasore Shycom,Kituo cha mabasi Mjini Shinyanga,Ibinzamata na Soko kuu,Nguzo nane Sokoni,Soko la Kambarage-Sanzugwanko,Voda shop na Brorisa Hotel",alifafanua  Rugora.

"Milango itakayotumika itakuwa mitano,jukwaa kuu watatumia Namba 1 na 2,nyuma ya jukwaa kuu,mlango namba 4,6 na 8 kwa wale wa mzunguko na mlango namba 5 utatumika kwa ajili ya magari maalum,Pikipiki na baiskeli za watazamaji hazitaruhusiwa kuingia uwanjani,watapaki eneo la uwanja wa Sabasaba au Kambarage ndogo jirani kabisa na Uwanja wa CCM Kambarage",aliongeza.

Akizugumzia kuhusu suala la ulinzi na usalama Rugora alisema wamejipanga vyema kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha mchezo huo unakuwa salama.

Na Kadama Malunde-Shinyanga
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
LIKE PAGE YETU HAPO PIA SHARE STORY NA RAFIKI ZAKO

0 comments:

Post a Comment

BURUDANI

 
Top