Mwanamke aliyebadili jinsia yake ya kiume na kuwa mwanamke na kutaka
jina lake kubadilishwa kwenye cheti chake cha mtihani ameshinda kesi
yake dhidi ya baraza la kitaifa la mitihani nchini Kenya.
Mahakama imelazimisha baraza hilo kumpa Adrey Mbugua cheti kipya
kinachoonyesha hali yake mpya ya kijinsia hasa kwa kuwa anapokea
matibabu ya kufanikisha jinsia yake kubadilika kabisa.
Bi Mbugua alilishitaki baraza la kitaifa la mitihani nchini humo kwa
kukataa kubadililisha utambulisho wa jinsia yake kwenye cheti hicho
kutoka kwa Mwanamme na kumtambua kama mwanamke licha ya amri iliyotolewa
katika gazeti rasmi la serikali.
Jaji Weldon Korir amelipatia baraza hilo hadi siku 45 kubadilisha jina
la Adrey katika cheti hicho kutoka kwa 'Andrew Mbugua' na utambulisho wa
mwanamume na kulibadilisha kuwa jina la kike la 'Audrey Mbugua' bila ya
kuweka jinsia yoyote.
Jaji alisema kuwa jinsia ya Adrey kwenye cheti hicho haiongezi thamani
yoyote kwa matokeo yake wala alama alizopata Audrey na kuondolewa kwake
vile vile hakuna athari yoyote.
Aliongeza kuwa Audrey ameonyesha kuwa yuko tofauti na hivyo ndivyo anavyopaswa kutambuliwa.
'Audrey ni mwanadamu ambaye anajitambua kwama mwanamke wala sio kama mwanamume jinsia aliyozaliwa nayo,'' alisema jaji.
Jaji alisema kuwa katiba ya nchi inaamrisha watu kuwaheshimu wengine
kama ipasavyo bila ubaguzi wowote na kwamba heshima hiyo inahusu mambo
mengi ikiwemo mtu anavyotaka kutambuliwa.
Aliongeza kuwa ili Audrey kuhisi kuwa sawa anapaswa kukubalika kama
alivyo na kumyima haki hiyo ya kubadilisha jina lake katika chati chake
itakuwa ukiukwaji wa haki zake za kibinadamu.
Wakili wa Audrey, aliambia mahakama kuwa mteja wake alizaliwa na kasoro ya kijinsia na kwamba anaendelea kupokea matibabu.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment