TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 08.10.2014.
- MTU MMOJA AFARIKI DUNIA NA WENGINE KUJERUHIWA BAADA YA MAGARI MAWILI KUGONGANA.
- JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA RAIA NA MKAZI WA WA NCHINI ETHIOPIA KWA KOSA LA KUINGIA NCHINI BILA KIBALI.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTU
MMOJA ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE, UMRI ATI YA MIAKA 25 – 30
AMEFARIKI DUNIA WAKATI AKIWA ANAPATIWA MATIBABU BAADA YA GARI LENYE
NAMBA ZA USAJILI T.397 AQT AINA YA ISUZU LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA
DEREVA AITWAYE NOEL MAHENGE KUGONGANA NA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI
T.505 BYG/T.843 CUG AINA YA SCANIA LIKIENDESHWA NA DEREVA AITWAYE
GODFREY PHILIMON (37) MKAZI WA TUKUYU WILAYA YA RUNGWE.
AJALI
HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE 07.10.2014 MAJIRA YA SAA 09:45 ASUBUHI HUKO
CHAPWA, KATA NA TARAFA YA TUNDUMA, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA KATIKA
BARABARA YA MBEYA/TUNDUMA.
AIDHA,
KATIKA AJALI HIYO WATU WAWILI WALIJERUHIWA NA KULAZWA KATIKA HOSPITALI
YA SERIKALI TUNDUMA AMBAO NI 1. SHABANI KIPANDE (22) MKAZI WA UYOLE NA
2. MUDDY MSELEMU (25). CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI WA GARI T.397 AQT
AINA YA ISUZU. DEREVA ALIKIMBIA MARA BAADA YA AJALI NA JITIHADA ZA
KUMTAFUTA ZINAENDELEA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI
YA SERIKALI VWAWA – MBOZI.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA
MOTO IKIWA NI PAMOJA NA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI
ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA, ANATOA WITO KWA YEYOTE
MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO DEREVA ALIYEKIMBIA KUZITOA KATIKA MAMLAKA
HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
TAARIFA ZA MISAKO:
JESHI
LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA RAIA NA MKAZI WA NCHINI ETHIOPIA
AITWAYE SEYIM LATABO (45) KWA KOSA LA KUINGIA NCHINI BILA KIBALI.
MHAMIAJI
HUYO ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 07.10.2014 MAJIRA YA SAA 07:50 ASUBUHI
HUKO KATIKA STENDI YA MABASI – TUKUYU, KATA YA KAWETELE, TARAFA YA
TUKUYU MJINI, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA AMESHAFIKISHWA
MAHAKAMANI KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WAGENI KUFUATA TARATIBU ZA KUINGIA NCHINI ILI
KUEPUKA MATATIZO NA MADHARA YANAYOWEZA TOKEA.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
0 comments:
Post a Comment