Cristiano
Ronaldo amerejea tena njiani msimu huu mara baada ya kutokuwa na msimu
wa kuvutia sana mwaka jana kutokana na kuandamwa na mamivu aliyoyapata
mnamo mwezi september mwaka jana.
Magoli
yake matatu aliyoyafunga kwenye mchezo dhidi ya Deportivo La Coruna
siku ya jumamosi yaliyoisaidia klabu yake ya Real Madrid kupata ushindi
wa jumla ya magoli 8-2 yamemfanya afikishe idadi ya hat-trick 24 na
hivyo kumfanya ashike nafasi ya pili nyuma ya Alfredo Di Stefano
aliyefunga hat-trick takribani 28 huku akimpita Ferenc Puskas aliyefunga
hat-trick 23.
Hat-trick
hiyo inamfanya pia Ronaldo ashike nafasi ya pili katika orodha ya
wachezaji waliowahi kufunga magoli matatu kwenye michezo ya La Liga
ambapo Di Stefano aniishikiria na nafasi ya pili ikienda kwa ligendari
wa klabu ya Athletic Bilbao Telmo Zarra aliyefunga hat-trick 22, wakati
mchezaji wa zamani wa Dunia anayekipiga ndani ya klabu ya Barcelona
Leonel Messi akiwa amekwishafunga mara 19.
Kwenye
michuano ya Uefa Champions League Ronaldo alivunja rekodi ya kufunga
takribani magoli 17 alipoisaidia klabu yake hiyo kuandikisha rekodi ya
La Decima kwenye msimu wa 2013-2014 akiivunja ile ya mara 14 iliyowekwa
na Lionel Messi, na goli lake la juzi alilolifunga dhidi ya klabu ya Fc
Basel lilikua ni goli la 68 kwenye michuano ya Ulaya ikiwa ni magoli
matatu pungufu ya mfungaji anayeshikiria rekodi ya kufunga magoli mengi
kwenye michuano hiyo Raul Gonzalez Blanco mwenye magoli 71.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment