KLABU ya Barcelona imekubali kumsajili beki wa kulia Douglas Pereira kutoka Sao Paulo kwa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 3.19, vigogo hao wa Katalumya wamethibitisha jana. Uhamisho unaweza kupanda kwa Pauni Milioni 1.2 zaidi kwa ajili ya beki huyo mwenye umri wa miaka 24 kulingana idadi ya mechi atakazocheza katika klabu yake mpya. Pereira atajiunga na klabu hiyo ya La Liga kwa mkataba wa miaka mitano iwapo atafaulu vipimo vya afya wiki hii nchini Hispania. TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
LIKE PAGE YETU HAPO PIA SHARE STORY NA RAFIKI ZAKO

0 comments:

Post a Comment

BURUDANI

 
Top