Wazee wetu walishawahi kuneno kwamba;
Ukishangaa ya Mussa utayaona ya filauni! Ndivyo unavyoweza kuanza kusema
kuhusiana na tukio la kushangaza lililotokea Kijiji cha Udindila Wilaya
ya Bagamoyo mkoa wa Pwani.
Mchungaji wa Kanisa la EAGT
aliyetambulika kwa jina la Boniface Onesmo alijikuta akibubujikwa na
machozi mara baada ya kushuhudia mkewe Bi. Benta Boniface akijifungua
hirizi baada ya kushika mimba kwa kipindi cha miezi saba na nusu!
Akizungumza na mtangazaji wa Kipindi cha
Hatua Tatu cha 100.5 Times Fm, Edson Mkisi Jr, Mchungaji huyo alisema
kabla ya kutokea kwa tukio hilo mkewe amekuwa na matatizo ya kuharibika
kwa mimba za mara kwa mara na tangu kuhamia kwa eneo hilo la Udingila
Bagamoyo mkewe huyo hajawahi kuzaa mtoto hata mmoja angawa amekuwa
akishika mimba kila walipohitaji kuzaa.
“Kwa hakika Mungu ni mwema na sitaacha kuendelea kumsifu na kumuabudu,” alianza kueleza Mchungaji Onesmo.
“Zaidi ya mtoto huyu mmoja niliyemzaa
kabla ya kuhamia hapa, hivi sasa kila ninapotaka kuzaa mtoto mimba za
mke wangu zinaharibika na hadi muda huu mimba zaidi ya nne
zimeshaharibika na hii nyingine ndio amezaa hirizi!” Mchungaji Onesmo
alisimulia.
Aliezeza kuwa siku ya tukio, mkewe
kipenzi alianza kusikia uchungu tangu saa nne asubuhi na kadri muda
ulivyozidi kwenda ndivyo uchungu ulipozidi kuongezeka.
“Hali iliendelea hivyo hadi saa nne
usiku ambapo mkewe alihisi kabisa kupushi na mimi nilikuwa tayari
kumsaidia lakini wakati anaendelea kupushi mkewangu akawa anatoa haja
ndogo mara kwa mara na alitoa haja ndogo hadi ndoo nne ndogo zilijaa na
kumwaga nje.
“Baada ya hapo aliendelea kusikia
maumivu makali ya tumboni huku akihisi kuzaa lakini baadae aliposikia
mtoto anakuja na mimi kujiweka tayari kumzalisha niliona kitu kinatoka
kama mtoto kukivuta ikatoka hirisi ikiwa imefungwa kitambaa chenye rangi
chekundu na nyeusi!” anasema.
Aidha, kwa upande wa mkewe, alisema kama siki hiyo kungekuwa na sumu ya panya angekunywa afe akapumzike.
Akizungumze huku akilia, mama Dotto
(Benta), anasema siku ya tukio hilo roho yake ilinusa kaburi kama kama
kungekuwa na hata mafuta ya taa kwenye kopo angekunywa ili afe.
“Nilimuuliza mume wangu mara kadhaa
kama kwenye kopo kuna mafuta ya taa lakini aliniambia yote aliweka
kwenye kandiri (taa ya chemli) na hata nilipoangalia tunapoweka sumu
sikuiona….kwa hakika kama ningekiona kimoja wapo ningekunywa nife!
Nimetesema sana,” anasema mama Dotto.
Mama Dotto alisema pamoja na changamoto
zote anazokutana nazo Bagamoyo lakini hajafikiria wala hafikirii kwenda
kwa mganga wa kienyeji.
“Siwezi kwenda kwa mganga wa kienyeji
kwa sababu waganga ukienda wao huongeza tatizo kwa hiyo nitaendelea
kumuomba Mungu hadi atakaposikia maombi yangu,” anasema huku akiangalia na mumewe pamoja na majirani waliofika kumjulia hali.
0 comments:
Post a Comment