NA BARAKA MBOLEMBOLE
Ushabiki ni kitu cha kwanza
katika mpira wa miguu.
Shabiki ni mtu anayependa ‘
kupita kiasi’ kile anachokuwa
anashabikia. Kama huna
sehemu unayoshabia basi si
rahisi kupata ‘ ladha halisi ya
mpira waiguu’. Kupitia timu
nayoishabikia naweza kuona
makosa ya kiufundi,
kufurahia ushindi, na vilevile
kupata maumivu makali. Leo
hii, maisha ya furaha ya
mashabiki wa Manchester
United yapo katika mashaka,
ile furaha ya kushangilia
ushindi kila mwisho wa wiki
si ya kuaminika tena.
Lakini ni hapo shabiki
anaweza kuona mapungufu
ya timu yake, na pengine
akajiaminisha kuwa ‘ usajili
zaidi hauepukiki’. Kila mtu
anaona udhaifu wa United
hivi sasa. Baada ya kipigo
katika uwanja wa Old
Trafford kutoka kwa Swansea
City siku ya ufunguzi, United
ilisafiri hadi Kaskazini
Magharibi mwa England na
kuambulia sare ya kufungana
bao 1-1 na Sunderland
katika uwanja wa Stadium of
Right. United imefanikiwa
kumsaini kiungo mshambulizi
wa kimataifa wa Argentina,
Angl Di Maria kutoka Real
Madrid kwa ada ya rekodi
England, pauni million 60. Di
mAria amevunja rekodi ya
usajili iliyowekwa na
Fernando Torres Januari
mwaka 2011 alipojiunga na
Chelsea kwa ada ya pauni
million 50 kutoka Liverpool.
Kabla ya msimu wa ligi kuu
England kuanza, United
ilikuwa katika kipindi kizuri
cha maandalizi nchini
Marekani. Huko waliweza
kupata ushindi dhidi ya timu
za AS Roma, Inter Milan,
Real Madrid, Liverpool, kabla
ya kuishinda, Valencia siku
chache kabla ya kuanza kwa
msimu. Timu ilionekana bora
chini ya kocha mpya, Luis
Van Gaal. Wachezaji wa safu
ya ulinzi, Criss Smalling,
John Evance, na Phill Jones
walionekana kuimarika na
kucheza vizuri katika mfumo
wa 3-5-2 ambao unawapa
uhuru wa kushambulia na
kukabia katikati ya uwanja
walinzi wa pembeni.
Van Gaal ametokea
kuwaamini sana wachezaji
hao wa Kiingereza, lakini
baada ya kushuhudia safu
yake ya ulinzi ikiruhusu
mabao mawili katika uwanja
wa nyumbani dhidi ya
Swansea, Van Gaal
aliharakisha usajili wa mlinzi
wa kushoto wa Argentina,
Marcos Rojo kutoka klabu ya
Sporting Lisbon. Rojo ana
uwezo wa kucheza nafasi ya
ulinzi wa kati lakini wakati
huu Luke Shaw akiwa katika
majeraha, Van Gaal
alimuhitaji, Rojo kucheza
nafasi ya beki wa kushoto
ambayo kiungo, Ashley
Young alicheza katika
mchezo wa kwanza. Smalling
aliumia katika mchezo dhidi
ya Sunderland, na walinzi
wengine si wa kuaminiwa
moja kwa moja kwa sababu,
Jones na Evance wote ni
wachezaji wa ‘ wasiwasi’ ni
wachezaji wazuri lakini muda
wowote wanaumia.
Kuondoka kwa manahodha
wote wanne kwa mpigo ni
tatizo lakini tatizo zaidi ni
kuwa wachezaji watatu
walikuwa sehemu ya ulinzi.
Patrice Evra, Rio Ferdinand
na Nemanja Vidic hawa
walikuwa msingi wa timu
katika ngome. Van Gaal
hatajuta kuondoka kwa
wakongwe hao, lakini
mashabiki wataendelea
kuona mapengo yao katika
ngome ya United kama
hataingia sokoni kuongeza
walau mlinzi mmoja wa kati.
Safu hiyo imekosa kiongozi
sahihi, majukumu ambayo
yalikuwa yakifanywa na Rio,
Evra na Vidic.
Usajili wa Di Maria umekuja
wakati mwafaka. United
hushambulia na kumaliza
mechi kupitia pembeni ya
uwanja. Huo ndiyo
utamaduni wa kiuchezaji
katika timu hiyo na Sir Alex
Ferguson alifanikiwa kwa
sababu hiyo. Van Gaal
atapata shinda katika mfumo
aliokuja nao, lakini ujio wa
Di Maria unaweza kumsaidia
kwa sababu tayari ana
uhakika wa kuwa na winga
wa hatari ambaye anauwezo
wa kukimbia na mpira ama
bila mpira katika eneo la
pembeni ya uwanja. United
ina uhakika wa kufunga
mabao, lakini safu ya ulinzi
haina uwezo mkubwa wa
kulinda lango lao. Van Gaal
ametumia pauni millioni 60
kumsaini, Di Maria, pauni
millioni 16 kwa Rojo, na
pauni millioni 17 kwa Shaw,
wote hao hawajatia mguu
uwanjani hivyo kuna
uwezekano mkubwa
wakainyanyua timu hiyo
kuanzia wikendi ijayo, ila
usajili wa nyongeza katika
ngome utasaidia kuziba
nyufa za wachezaji
wanaokumbwa na majeraha
ya mara kwa mara. Usajili
wa bei mbaya wote
ulichemsha England, Juan
Sebastian Veron, Robinho,
Fernando Torres, ila sitaraji
hivyo kwa Di Maria.
0714 08 43 08
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
LIKE PAGE YETU HAPO PIA SHARE STORY NA RAFIKI ZAKO
0 comments:
Post a Comment