Mwili wa Rashid Athuman ukiwa unaning’inia katika kitanzi ambacho alikifunga chooni kabla ya kujinyonga kasha kujifungia chooni.
Mwili wa Rashid Athuman ukishushwa na wasamaria wema kutoka kwenye kitanzi kwa kwa kushirikiana na Jeshi la polisi.
Mwili wa Rashid Athuman ukiwa unahifadhiwa katika chumba cha kuhifadhiwa maiti katika hospital ya Peramiho.
Hiki
ni chumba ambacho marehemu alikuwa amepanga na kinachoonekana ni
kitanda ambacho alikuwa anatumia kulala yeye na mke wake .
Mke wa marehemu Lucy Adam (24) akiwa amembeba mtoto wake Yoweri Rashid (02) mgongoni.
--------------------------------
Na Oswad Ngonyani wa demashonews. Peramiho - Songea
Ikiwa
imepita siku moja tangu mazishi ya Fundi maabara mstaafu wa Hospitali
ya Peramiho Bwana Frederick Mgaya (60) ambaye alifariki kwa kujinyonga
alhamisi iliyopita hapa Peramiho, mtu mwingine tena aliyetambulika kwa
jina la Rashid Athuman (32) amekutwa amejinyonga katika choo cha nyumba
aliyokuwa akiishi.
Bwana
Rashid Athuman ambaye ni mkazi wa Usangu Jijini Mbeya amejinyonga kwa
kutumia shuka majira ya saa Saba za usiku baada ya kumuaga mke wake Bi
Lucy Adam (24) kuwa anakwenda chooni kujisaidia ambapo alikwenda
kukamilisha mpango wake huo.
Taarifa
kutoka kwa mke wake huyo zinaeleza kuwa enzi za uhai wake Bwana Rashid
Athuman alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kifua kikuu, tatizo
lililowafanya wachukue uamuzi wa kuja Peramiho kwa ajili ya matibabu.
Bi
Lucy anazidi kutanabaisha kuwa walifika Peramiho tarehe 19 Mwezi Julai
2014 na kupata chumba cha kupanga katika Kitongoji cha Namihoro jirani
na Stendi Kuu ya Peramiho katika nyumba ya Cosmas Chidumule ambapo tangu
wakati huo waliendelea na maisha yao wakiwa wakisaidiwa chakula na
majirani waliokuwa na mapenzi mema.
“Tangu
jana asubuhi nilishinda vizuri tu na marehemu mume wangu ambapo mishale
ya saa tatu za usiku tulienda kulala. Muda mchache baadaye nilipitiwa
na usingizi mpaka majira ya saa saba za usiku ambapo marehemu aliniamsha
na kunieleza kuwa alikuwa anakwenda uani kujisaidia ambapo baada ya
yeye kuelekea uani mimi niliendelea kulala” Alisema mke huyo wa
marehemu.
“Baada
ya muda mrefu kupita pasipo marehemu kurudi nikaamua kuamka na kutaka
kuufungua mlango wa chumbani lengo hasa likiwa kwenda uani kujua sababu
ya mume wangu kuchelewa kurudi. Nilishangaa kuona mlango umefungwa kwa
nje na ikanibidi nitumie kisu ili kuweza kuufungua mlango huo ambapo
nilifanikiwa na kwenda uani ambapo nilikuta mlango wa uani ukiwa
umefungwa kwa ndani kitu kilichonifanya niusukume kwa nguvu na kumkuta
mume wangu akiwa ananing’inia huku akiwa amekwishafariki” Alimalizia
mjane huyo.
Mjane
huyo ameishi na marehemu kwa muda wa miaka mitatu na kufanikiwa kupata
mtoto mmoja wa kiume, Yoweri Rashidi (2) ambapo uchunguzi zaidi kuhusu
chanzo cha kifo hicho bado unaendelea.
0 comments:
Post a Comment