B Assemblies of God jijini Dar, Dk. Getrude
Rwakatare (pichani) amefunguliwa mashitaka
katika Kituo cha Polisi Wazo Hill kwa uharibifu wa
mali inayodaiwa ina thamani ya shilingi milioni 20.
Bw. Grayson Justine anayelalamika kuvunjiwa
nyumba yake na Mch. Getrude Rwakatare.
Taarifa zilizopatikana katika kituo hicho zenye
Jalada la Kumbukumbu WH/RB/9029/2014
UHARIBIFU WA MALI na kuthibitishwa na
mlalamikaji aliyejitambulisha kwa jina la Grayson
Justine, zinaeleza mchungaji huyo alivunja nyumba
ya Grayson kwa greda hali iliyomfanya mmiliki
huyo kuzimia na kulazwa Zahanati ya Mico iliyopo
Wazo Hill baada ya presha kupanda.
Katika mahojiano na waandishi wetu katika Ofisi za
Global Publishers, Bamaga- Mwenge, Dar wiki
iliyopita, Grayson alikuwa na haya ya kusema:
Nyumba ya Bw. Grayson wakati wa ujenzi.
“Kiwanja nilichojengea nyumba nilikinunua kwa
Jumanne Rajab, Agosti 24, 2011 na makubaliano
yalifanyika kwa kuandikishiana Ofisi za Serikali ya
Mtaa wa Bunju ‘B’ na kila mmoja alikuwa na
mashahidi wake.
“Kutokana na kuchoka katika kupangisha, niliamua
kuchukua mkopo wa shilingi milioni 20 kazini ili
nijenge haraka na kuhamia, ujenzi ulianza
Septemba 21, mwaka 2013 mpaka kufikia mwezi
huu (Novemba) nilibakiza kupaua na nilitarajia
kuhamia mwanzoni mwa mwaka kesho.
Mabaki ya matofali ndani ya uzio wa Nyumba ya
Bw. Grayson Justine iliyobomolewa kwa greda.
“Baadaye nilikwenda Moshi kwenye msiba wa
baba, niliporudi Dar nilimaliza siku moja tu,
nikaripoti kazini. Nikiwa kazini Novemba 11,
mwaka huu nikapigiwa simu na jirani kwamba
nyumba yangu inabomolewa na greda, alifikiri
kwamba nimeshaonana na Mchungaji Rwakatare
na kukubaliana naye.
“Nilikwenda kule, kufika nikakuta hakuna jengo!
Nilidondoka chini, sikujua kilichoendelea, nilipoteza
fahamu, nilijitambua nikiwa Zahanati ya Mico.
“Kinachoniumiza sana ni kitendo cha kuvunjiwa
nyumba yangu bila kushirikishwa, bora hata
angenifungulia mashitaka kama anaona nilivamia
kikwanja chake.”
“Yeye ana uwezo, ana ghorofa ya zaidi ya shilingi
bilioni moja iweje anionee na kunivunjia mimi
maskini niliyejenga kwa fedha za mkopo?
“Kituo cha polisi nilifika karibu mara nne lakini
mpaka leo hii sijapewa mpelelezi wala hawajafika
eneo la tukio, nataka sheria ichukue mkondo
wake.”
Mwandishi alifika katika eneo la tukio na
kushuhudia kifusi kinachodaiwa kuwa ni iliyokuwa
nyumba ya Grayson iliyovunjwa na imezungushiwa
ukuta na geti kupigwa kufuli.
Hata hivyo, Uwazi lilifika katika Ofisi za Serikali ya
Mtaa wa Bunju ‘B’ na kuonana na mtendaji
Abdallah Mkeyenge ambaye alikiri kuwepo kwa
mvutano baina ya watu hao.“Hii barua ya
makubaliano ya kuuziwa Grayson kiwanja
inaonekana imetoka ofisini hapa lakini mimi kipindi
hicho nilikuwa sijahamia ofisi hii.
Jumba la kifahari la Mch. Getrude Rwakatare.
“Ninachokumbuka kuna kipindi Mchungaji
Rwakatare alikuja na milioni tano kuwapa Grayson
na mtu mwingine yaani kuwapoza lakini walikataa
kuzichukua,” alisema mtendaji huyo.
Mchungaji Rwakatare alipopigiwa simu kuhusiana
na madai hayo alisema yupo bungeni hivyo
alimwagiza msaidizi wake, Jerad Abeid
kuzungumzia sakata hilo ambapo alisema eneo hilo
mchungaji analimiliki tangu mwaka 2005 na hati
ziko ardhi Wilaya ya Kinondoni. Alibomoa nyumba
ya Grayson akijua ni eneo lake la siku nyingi.
“Unajua katika maeneo hayo kuna watu walikuwa
wakishirikiana na ofisi za mtaa kuuza kiwanja cha
mchungaji kwa siri na tayari watu wanne
walishauziwa lakini walikuwa hawajajenga,
mchungaji aliamua kuwapoza kiubinadamu na
wameshaondoka bado watu wawili akiwemo huyo
Grayson,” alisema Jerad.
Related Posts
MAPENZI BHANA! DIAMOND AANIKA SABABU 5 ZA KUMPENDA ZARI! KUMTAMBULISHA X-MASS, AWACHAMBUA MA-EX WAKE!
Mapenzi bhana! Baada ya kutoka kimalavu na kumwagana na mwanadada mwenye mvuto Bongo, Wema Isaac Se[...]
Wema Sepetu Amfuata Diamond Platnumz Kampala Uganda...Je Wawili Hawa Wanafuatana au Wanarushana Roho? Usiku wa juzi tarehe 18, jiji la Kampala nchini Uganda lilipambwa na “EVENTS” mbili mkubwa kwenye upande wa buruani ambazo ni Show kubwa ya mwnamziki Jose Chameleone iliyofahamika kama 1Man Show Million na Pati ya mwanamama Zari iliyofahamika kama Zari All White Ciroc Party. Mwigizaji Wema Sepetu na mwanamziki Diamond Platnumuz wote walitua nchi humo na kugawana matukio hayo kama ifuatavyo; Wema Sepetu ambae anadai ni amekuwa shabiki mkubwa wa masanii Jose Chameleone alitokea nchini Ghana na kutua jijini Kampala kuhudhuria show ya mwanana mziku huyo ambayo ilifanyika Serena Hotel. Wakati Diamond Platnumz ambae kwasasa ana “Le Project” na mwanamama Zari alihudhulia pati ya Zari kama “Special Guest”. Baadhi ya watu wamechukulia kitendo hiki ni kama mwanadada Wema “Amepaniki” hivi, Huku wengine wakisema kuwa Wema ana uhuru wakufanya kile anachokitaka bila ya kuhofia watu watasemaje. Jambo hili halijatokea kwa bahati mbaya kwani wiki kadhaa zilizopita, Diamond alipoonyesha kum- support Zari kwenye pati yake,Wema nae alibuka na kum-support Jose. Kama unavyoona hapa chini. Maoni yako tafadhari, Je wawili hawa wanatafutana au wana rohorushana
Usiku wa juzi tarehe 18, jiji la Kampala nchini Uganda lilipambwa na “EVENTS” mbili mkub[...]
Staa huyu wa Nollywood aeleza sababu za kwa nini hayupo tayari kuingia katika maisha ya ndoa kwa sasa
Mwigizaji wa Nollywood Genevieve Nnaji amefunguka kuhusu hatma ya maisha yake ya ndoa na kueleze[...]
AT ASHINDA KESI DHIDI YA MGANGA WA JADI ALIYEMSHITAKI KWA KUTOMLIPA PESA BAADA YA KUPANDISHA NYOTA YAKE
Muimbaji wa Mduara, AT ameshinda kesi iliyokuwa ikimkabili nailiyofunguliwa na mganga wa jadi k[...]
PICHAZ: UNAAMBIWA HUYU NDIYE MBUNGE MZURI KULIKO WOTE NCHINI KENYA
Anajulikana kwa jina la Naisula Lesuuda ambaye aliwahi kuwa mwandishi wa kituo cha Tv kenya cha KBC [...]
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment