Aibu kuu! Jamaa aliyejitambulisha kwa jina la Leonard Celestine ambaye anasomea upadri, anayemalizia masomo ya falsafa (philosophy) mwaka wa tatu katika Chuo cha Jordan mjini Morogoro, anadaiwa kuaibika gesti, kisa kikiwa ni mke wa mtu gesti.
Bw. Leonard Celestine aliyeaibika gesti na mke wa mtu.

TUJIUNGE GESTI

Kwa mujibu wa shuhuda wetu, tukio hilo la aina yake lilijiri hivi karibuni kwenye Gesti ya Silver Inn iliyopo maeneo ya Msamvu mjini Morogoro ambapo kijana huyo alipewa kipondo cha aina yake na kunyang’anywa kila kitu huku akiachwa kama alivyozaliwa na kulazimika kujisitiri na taulo la nyumba hiyo ya wageni.

KITU LAIVU!

Chanzo hicho kilidai kwamba, kijana huyo ambaye ni mwenyeji wa Iringa alikuwa na mchezo wa kutembea na huyo mke wa mtu tangu mwaka jana ambapo mumewe aliamua kumwekea mtego ulipofyatuka akanaswa laivu.

Bw. Leonard Celestine akijutia soo lililomkuta.


KUMBE!

Ilidaiwa kwamba, kama ilivyo seminari zote za Kikatoliki, mwanafunzi hutakiwa kukaa ndani lakini Leonard alidaiwa kuwa alikuwa akitoroka hasa siku za wikiendi au siku akiwa na vipindi vinavyoishia asubuhi na kwenda kukutana na mke huyo wa mtu na kujiachia naye kwani mumewe ni mtu wa kusafiri mikoani.
Ilisemekana kuwa kutokana na kujiachia huko mwenye mke aligundua na kuanza kumfuatilia tangu mwaka jana hadi alipowanasa hivi karibuni.

KIPIGO

Baada ya kunaswa, Leonard alipewa kipigo cha aina yake na watu ambao tayari walikuwa wameshaandaliwa na mwenye ‘mali’ ambapo alilia huku akiomba asamehewe ili yasije kuvuja akakosa upadri kwani ameshafika mbali.

Bw. Leonard Celestine akibanwa kwa maswali mara baada ya kupewa taulo kujisitiri.

APOKONYWA KILA KITU

Ilidaiwa kwamba, raia hao wenye hasira walimpokonya simu, begi lake lililokuwa na madaftari na nguo hivyo alitoka chumbani bila nguo na badala yake aliomba taulo kujisitiri.


PADRI ANASEMAJE?
Gazeti hili lilimtafuta Leonard kwa njia ya simu aliposomewa mashtaka yake alisema:
“Ni kweli hizo picha ni zangu, nalijua hilo tukio lakini ndugu mwandishi naomba usinitoe, nitakuwa nimekwisha kwani yule mwanamke hakuniambia kama ni mke wa mtu.”
Source GPL
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
LIKE PAGE YETU HAPO PIA SHARE STORY NA RAFIKI ZAKO
Next
MICHEPUKO SIO DILI: DIWANI MTARAJIWA ANASWA NA DENTI GESTI
Previous
Belle 9 Hataonekana kwenye wimbo mpya alioshirikishwa na Young Killer na Fid Q '13', Msodoki atoa Sababu soma hapa Wimbo mpya wa Young killer aliomshirikisha kaka yake kiumri na kimuziki Farid Kubanda aka Fid Q na Belle 9 '13'  umetambulishwa rasmi jana kwenye vituo mbalimbali vya redio. Habari Njema kwa mashabiki wa Msodoki ambao wameupokea vizuri wimbo huu ni kuwa video ya "13"iliyoongozwa na Director Nisher pia imekamilika na inatarajiwa kutoka soon. Lakini habari mbaya kuhusu video hiyo ni kuwa Belle 9 ambaye amesikika kwenye kiitikio cha wimbo huo hataonekana kabisa kwenye video. Msodoki amekanusha maneno yaliopo mtaani kuwa walishindwa kuelewana na Belle hadi kushindwa jutokea kwenye video hiyo. "Haya maneno sidhani kama ni ya kweli" Amesema Young Killer kupitia kipindi cha Power Jams ya  East Africa Radio, "kwa sababu Belle ni mtu ambaye tuko nae na hii ngoma imefanyika kama wiki mbili nyuma, na baada ya kufanyika wiki mbili nyuma zikapita siku mbili tukafanya video. Kwa hiyo ndani ya wiki mbili nyuma ukitoa siku mbili hizo tulikuwa nae Bongo records yumefanya ngoma, lakini ni time ambayo ilikosekana kutokana na yeye pia alikuwa katika kutambulisha wimbo wake wa Vitamin Music, so tour zake za media nadhani kidogo zilikuwa zimebanana" Msodoki Ameongeza kuwa hadhani kama kutokuwepo kwa belle kama kutaathiri kwa vyovyote video yake. "Kitu ambacho naamini itatuaffect kwa mawazo lakini tutaitazama naamini watu wote tutaenjoy kutokana na sauti yake ipo na yeye pia tumem mention".

0 comments:

Post a Comment

:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

BURUDANI

 
Top