STAA wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper Masawe ‘Jack
Wolper’ amejikuta akitumika kwenye utapeli wa mamilioni ya shilingi
kupitia mitandao ya kijamii bila yeye kujua,limeinyaka.
Akizungumzia
sakata zima huku alibubujikwa na machozi, Wolper alisema: “Siku moja
nilikutana na dereva teksi mmoja aitwaye Ismail, baada ya kupiga stori
nilimpa namba yangu ya simu na yeye akanipa yake, tukaagana.
Staa wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper Masawe ‘Jack Wolper’
“Siku chache baadaye Ismail akanipigia simu na kuniuliza kulikoni
naomba sana watu wanisaidie pesa kwenye WhatsApp kwa ahadi ya
kuwarejeshea?“Akaniambia kama nina tatizo bora wakati mwingine
nimshirikishe kuliko kila kukicha kuombaomba pesa.
“Hapo ndipo nikagundua kuna mtu kajisajili kwa jina la Jacqueline
Masawe na hata kwenye namba nyingine za simu anazotumia kuomba watu
pesa, amejisaliji kwa jina hilohilo.“Pia kwenye Facebook, WhatsApp
anatumia picha zangu, hapo ndipo nikagundua kuwa, kuna mtu anatapeli
watu kupitia jina langu,” alisema Wolper.
Staa wa filamu, ‘Jack Wolper’ akipozi.
Akaongeza kuwa, baada ya kugundua utapeli huo akashangaa wanajitokeza
watu wakisema wanamdai ambapo imebainika mtu huyo alikuwa kakopa pesa
kwa watu tofauti zinazofikia shilingi milioni 10 lakini wengi
walimuelewa hivyo kuripoti tukio hilo kwa vyombo vinavyohusika ili
kumsaka mtuhumiwa.
TAHADHARI YA MHARIRI
Baadhi ya watu wamekuwa wakitapeli kupitia
njia ya mtandao hivyo ni vyema kila mmoja kuwa makini ili kuepukana na
matatizo kama yaliyomkuta Wolper.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
LIKE PAGE YETU HAPO PIA SHARE STORY NA RAFIKI ZAKO
0 comments:
Post a Comment