Dk. Antony Dialo, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza
Chama cha
Mapinduzi (CCM), mkoani hapa, kimekemea siasa za kuchafuana zinazofanywa
na Mwenyekiti wa CCM, mkoa wa Mwanza, Dk. Antony Dialo dhidi ya Waziri
Mkuu mstaafu, Edward Lowassa.
Kimesema
mwenyekiti huyo akizungumza na baadhi ya vyombo vya habari, alisema
Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, hakufanya kazi ya kuleta maji ya
Ziwa Victoria na kuyasambaza mkoani Shinyanga. Akizungumza juzi na
waandishi wa habari, Katibu wa siasa na uenezi mkoani Shinyanga,
Emmanuel Mlimandago, alisema kauli ya Dialo ni ya ulimbukeni wa kisiasa
na kujitafutia umaarufu kupitia mgongo wa Lowassa.
Alisema
amekuwa akisoma taarifa mbalimbali kupitia kwenye vyombo vya habari,
akimtuhumu na kumtolea kashfa waziri mkuu huyo mstaafu.
“Mimi kama
katibu mwenezi wa CCM, mkoani Shinyanga nilishuhudia mradi huo wa maji
kutoka ziwa Victoria na kuletwa mjini Shinyanga enzi za waziri mkuu huyo
mstaafu na kipindi hicho Dialo alikuwa naibu waziri wa maji,” alisema.
Alisema kwa
kawaida kazi anazozifanya naibu waziri ni maagizo kutoka kwa waziri
mwenye dhamana, hivyo Dialo alikuwa mtu wa kuagizwa na Lowassa
kutekeleza majukumu hayo.
“Kwa niaba
ya CCM mkoani Shinyanga, tunakemea kitendo alicho kifanya Dialo cha
kumchafua Edward Lowasa na tunamuonya tabia hiyo isijirudie na aache
upotoshaji huko ni kujitafutia umaarufu na heshima asizo stahili kupitia
mgongo wa Lowassa” alisema.
Aliongeza
kwa maneno aliyoyasema Dialo, na majigambo ni dhahiri kuwa ameonyesha
udhaifu wa hali ya juu na amewadhalilisha wasomi wenye elimu kama yake
ya PhD, na kuonyesha elimu yake ni ya mashaka kwa kutokujua kuchambua
mambo yeye kama msomi. Mlimandago, alisema kuwa inawezekana Dialo
anatumiwa na baadhi ya wanasiasa kwa kumchafua Lowassa kutokana na
kutangaza nia ya kugombea urais mwakani.
0 comments:
Post a Comment