Wasichana
saba wamepoteza maisha wilayani Nachingwea mkoani Lindi baada ya
kubakwa na kunyongwa kisha kuwekewa vijiti na chupa kwenye sehemu zao za
siri.
Wasichana
hao wamepoteza maisha kwa nyakati tofauti katika kipindi cha miezi
minne iliyopita na wamekuwa wakipigiwa simu nyakati za usiku na kukutana
na waliowapigia simu ambapo hubakwa na kunyongwa na kisha katika sehemu
za siri kuwekewa vijiti au chupa.
Mkuu
wa Mkoa wa Lindi, Ludovick Mwananzila amebainisha aina hiyo ya mauaji
jana wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika
Hospitali ya Mkoa ya Sokoine.
Mwananzila
alikuwa amekwenda hospitalini hapo kuwatazama majeruhi ambapo
alifafanua kuwa mauaji hayo yanaendelea na juzi mtu mwingine aliuawa
katika mazingira hayo.
Alisema, “serikali
ya wilaya ilishatoa namba za simu kuwa unapopigiwa simu mtoto wa kike
fanya juhudi kumjulisha mwenzako au piga simu kituo cha polisi ili
kuweza kukabiliana na watu hao wanaotoa roho za watu”.
Mwananzila
alisema kuwa binti mmoja aliweza kupigiwa simu na kundi hilo, aliamua
kupiga simu kituo cha polisi na kuweka mtego baada yeye kutoka nje,
polisi walikuwa wameshazingira maeneo hayo na wauaji wale walimfuata
ndipo huyo binti alianza kuvutana nao na hatimaye Polisi waliwatia
mbaroni watu hao.
Mkuu huyo wa mkoa aliwaonya mabinti hao na kusema: “ni makosa kwa wasichana kutoka nje baada ya kupigiwa …
“kinachotakiwa kwanza mjulishe mwenzako, lakini unafanya siri madhara yataweza kukutokea, hususani watoto wa kike”.
Alisema mauaji hayo yana ishara ya imani ya kishirikina. Hata hivyo uchunguzi unaendelea kufanyika.
Alisema suala hilo liko ndani ya uchunguzi hivyo ni vizuri kufanyia kazi kwanza na kuwataka wananchi wawe na subira.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.