Miss Tanzania 2013 akitokea Miss Ilala,
Martha Gewe, mkazi wa Tabata Segerea, Dar
amefariki dunia baada ya kuugua ghafla, Ijumaa
Wikienda linakupa zaidi.
KWELI
Martha amekutwa na mauti katika Hospitali ya
Mkoa wa Ilala, Amana jijini Dar es Salaam,
Ijumaa iliyopita ambako alikimbizwa baada ya
kuugua na madaktari walibaini kwamba,
malaria ilipanda kichwani.
Marafiki wa aliyekuwa mshiriki wa Miss
Tanzania 2013 akitokea Miss Ilala, Martha
Gewe wakiwa na huzuni.
AFYA YAKE SIKU ZA NYUMA
Habari zaidi zinasema kuwa mrembo huyo
hakuwa akisumbuliwa na ugonjwa wowote huko
nyuma na alionekana mwenye afya njema huku
mipango yake ikiwa imelenga jinsi
atakavyoisherehekea Sikukuu ya Krismasi.
“Lakini Jumatano iliyopita alianza kuumwa,
alisema anahisi homa ambayo baadaye
ikabainika ni malaria.
Mwili wa marehemu Martha Gewe ukiwa
kwenye jeneza.
“Tulimpeleka Amana, akalazwa kwa siku tatu
tu, leo (Ijumaa) akafariki dunia. Madaktari
wamesema ile malaria kukimbilia kichwani
ndiyo tatizo,” alisema ndugu mmoja wa
marehemu huyo kwa sharti la kutochorwa jina
gazetini kwa kuwa siyo msemaji wa familia ya
mzee Gewe.
WALICHOSEMA MADAKTARI
Ijumaa Wikienda lilifanikiwa kuzungumza na
madaktari wawili wa Hospitali ya Amana jijini
Dar kuhusu ugonjwa wa malaria kupanda
kichwani.
Na hii ndio safari ya mwisho ya marehemu
Miss Martha Gewe.
“Mpaka sasa bado malaria ni tishio, inaua watu
wengi sana. Kwa malaria kupanda kichwani ni
hatari zaidi kwani mgonjwa anaweza kupoteza
maisha ndani ya muda mfupi sana.
“Kikubwa watu wazingatie kuwa mbali na
mazingira hatarishi kwa ugonjwa huo na
wajichunge kuumwa na mbu ambao ndiyo
wana-oeneza ugonjwa huo,” alisema daktari
mmoja.
Kufuatia taarifa za kifo hicho, mamisi wenzake
walipigwa na mshangao, wengine wakiuliza nini
kilimpata mwenzao huyo!
MAMISI WENZAKE NI MACHOZI
. Miss Tanzania 2013 Happiness Watimanywa
“Kwa kweli nilipopata taarifa za kifo cha Martha
sikuamini mara moja kwa vile sijawahi kusikia
akiumwa au hata kwamba alilazwa kwa muda
mrefu.
“Kifo chake kimeniumiza sana, sijui hata
nisemeje jamani, kweli kifo hakina huruma,”
alisema Miss Ilala 2013, Dorice Mollel huku
akilia.
Mrembo mmoja ambaye hakutaja jina lake
alisikika akisema: “Yaani Happiness
(Watimanywa) yuko Uingereza kusaka taji
mwenzake anapoteza maisha ghafla hapa
nyumbani Tanzania! Inauma sana kwa kweli.”
Warembo wengine walioshiriki msiba wa
Martha nyumbani kwao, Tabata, Dar
walishindwa kujizuia na kujikuta wakibubujikwa
machozi muda wote kiasi cha kushindwa
kuongea na mwandishi wa gazeti hili.
Hashim Lundenga ‘Anko’.
HISTORIA YA MARTHA KATIKA UMISI
Mwaka jana, Martha alishiriki shindano la
kumsaka Redd’s Miss Ukonga lililofanyika
katika Ukumbi wa Wenge Garden, Ukonga
Mombasa jijini Dar.
Katika kinyang’anyiro hicho, Martha aliibuka
kidedea kwa kuvalishwa taji hivyo kupata tiketi
ya kwenda kushiriki Miss Ilala 2013 kwenye
Ukumbi wa Golden Jubilee Tower, Dar ambapo
mshindi alikuwa Dorice.
Marehemu alipata nafasi ya kuvuka Miss Ilala
na kushiriki Redd’s Miss Tanzania 2013 chini
ya Hashim Lundenga ‘Anko’ na kufanikiwa
kuwa miongoni mwa Kumi Bora huku
Happiness Watimanywa akiibuka mshindi.
Marehemu Martha Gewe enzi za uhai wake.
Watimanywa usiku wa kuamkia leo, kule jijini
London, Uingereza alifurukuta kugombea Taji
la Miss World!
MAZISHI YA MARTHA
Marehemu Martha alizikwa Jumamosi iliyopita
kwenye makaburi ya nyumbani kwao, Tabata
Segerea jijini Dar es Salaam huku msiba huo
ukihudhuriwa pia na warembo mbalimbali
ambao wamewahi kuvaa mataji nchini.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment