Kuonesha
wapo ‘serious’ na mavazi, polisi walimtaiti staa wa Bongo Fleva, Rashid
Makwiro ‘Chid Benz’ na kumtaka akavae vizuri kisha arejee mahakamani.
Tukio
hilo lilitokea juzi, Jumanne katika Makahama ya Hakimu Mkazi Kisutu
jijini Dar, wakati staa huyo alipokuwa amefikishwa kusomewa mashtaka
yake ya kukutwa na madawa ya kulevya.
Akiwa
katika viunga hivyo vya mahakama, Chid Benz alionekana akiwa ametinga
jinzi ambayo ililegezwa mkanda na alipoingia ndani ya chumba cha
mahakama, mlegezo uliongezeka zaidi hadi kufikia chini ya makalio
kitendo ambacho polisi walishindwa kukivumilia.
Kuonesha kwamba hawakufurahishwa na kitendo hicho, maafande waliokuwa wakimsindikiza Chid mahakamani hapo, walimtaiti kwa kumshika kiunoni na kumtoa nje kwenda kumpandisha suruali hiyo kisha kumrudisha akiwa amevaa vizuri.
Akiwa
mahakamani hapo mbele ya Hakimu Waliarwande Lema na mwendesha mashtaka,
PP Mwanaamina Komba, Chid alisomewa mashtaka matatu aliyokutwa nayo
Oktoba 24, mwaka huu katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini
Dar.
Mashtaka hayo ni; kukutwa na madawa ya kulevya aina ya heroin gramu 0.25 yenye thamani ya Sh. 38,638, bangi gramu 1.72 ambayo thamani yake ni Sh. 1,720 na vifaa vya kuvutia (kifuu cha nazi na kijiko).
Mashtaka hayo ni; kukutwa na madawa ya kulevya aina ya heroin gramu 0.25 yenye thamani ya Sh. 38,638, bangi gramu 1.72 ambayo thamani yake ni Sh. 1,720 na vifaa vya kuvutia (kifuu cha nazi na kijiko).
Chid
aliyakana mashtaka yote matatu hakimu akaahirisha kesi hiyo hadi
Novemba 11, mwaka huu na kuweka dhamana wazi ya faini ya shilingi
milioni moja na wadhamini wawili lakini mshtakiwa hakukidhi masharti ya
dhamana, akaomba kukamilisha masharti hayo kesho yake (Jumatano) hivyo
akarudishwa mahabusu Segerea.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment