CHEREKO chereko! Siku
chache baada ya supastaa ‘grade one’ wa sinema za Bongo, Wema Sepetu
‘madam’ kummwaga King of Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, mama mzazi
wa mwigizaji huyo, Mariam Sepetu ameangusha sherehe ya nguvu kama
ishara ya kuonesha ‘amekunwa’ na tukio hilo, Ijumaa Wikienda linashuka
nayo mstari kwa mstari.
Supastaa ‘grade one’ wa sinema za Bongo, Wema Sepetu ‘madam’ akipozi.
TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa
mujibu wa chanzo makini, kutokana na mama huyo kutobariki uchumba wa
mwanaye na Diamond ambaye pia anajulikana kwa jina la Dangote kwa muda
mrefu, habari za uchumba huo kuvunjika zilipochapishwa kwenye Gazeti la
Ijumaa ‘Kubwa’ toleo lililopita, moyo wake ulijawa na furaha.
“Mama
Wema alichukizwa kwa kiasi kikubwa na mapenzi ya wawili hao kutokana na
kile alichoamini kuwa, Diamond hakuwa na mapenzi ya dhati kwa mwanaye
zaidi ya kutegemea nyota yake impe mafanikio ndiyo maana akafanya pati
hiyo fupi nyumbani kwake Sinza-Mori, Dar,” kilisema chanzo hicho.
Wema Sepetu ‘madam’ akifurahi na mama yake, Mariam Sepetu
SHEREHE ILIVYOKUWA
Chanzo
hicho kilizidi kumwaga unga kwamba, sherehe hiyo ilikuwa ni ya aina
yake kwani mama Wema aliwaita mashosti zake, wakaandaa ‘menu’ ya ukweli
kabisa, wakasherehekea lakini bahati mbaya Wema hakuhudhuria.
“Wema hakuweza kuhudhuria sherehe hiyo kutokana na kubanwa na majukumu mengine. Bi mkubwa aliwaita marafiki zake, wakafungua shampeni, wakala, wakanywa na kucheza muziki kufurahia Dangote kupigwa chini,” kilisema chanzo hicho.
MAMA NA CHUKI YA MUDA MREFU
Chanzo
hicho kilizidi kumwaga ubuyu motomoto kuwa, mama Wema alipiga
cherekochereko za kutosha siku hiyo kwani alikuwa akimchukia Diamond kwa
muda mrefu.
“Mama
Wema chuki zake kwa Diamond hazitaisha kamwe kwa kuwa hampendi tu
kutokana na kuona mwanaye hasongi mbele kimaendeleo kama alivyo Diamond
ambaye akiachana na Wema mambo yake hayamwendei vizuri kama anavyokuwa
na mwanaye.”
Diamond wakati akiwa na Jokate Mwegelo.
MAMA WEMA ANENA
Baada
ya wanahabari wetu kunasa maelezo hayo ya chanzo, walimvutia waya mama
Wema ambaye alikiri kufanya sherehe fupi baada ya mwanaye kummwaga
Diamond.
“Mimi
naona huu ndiyo mwisho wa Wema na Diamond na siku zote nasema hakuna
uhusiano ukadumu bila baraka za wazazi, niseme tu, sitaki kumuona ndugu
yeyote wa Diamond kwangu, kama mahari wakatoe kwa Penny siyo kwa
mwanangu,” alisema mama Wema.
Wema Sepetu,'Madam' akiwa na Diamond Platinumz.
TUJIKUMBUSHE
Kumwagana
kwa Wema na Diamond safari hii, ni mara ya nne. Awali walimwagana,
wakarudiana, wakamwagana tena, Diamond akatua kwa Jokate Mwegelo,
wakarudiana tena na Wema, wakaja mwagana tena, Diamond akatambaa na
Penniel Mungilwa ‘Penny’, wakamwagana, karudiana na Wema, sasa
wamemwagana tena.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment