MSHAMBULIAJI Wayne Rooney amemfikia kwa mabao gwiji wa Arsenal, Thierry Henry katika Ligi Kuu ya England baada ya Nahodha huyo wa Manchester United kufunga bao moja leo katika ushindi wa 4-0 dhidi ya Queens Park Rangers.
Mchezaji huyo wa England alifunga dakika ya 44 na kufikisha jumla ya mabao 175 aliyofunga katika Ligi Kuu ya England pekee.
Mabao mengine ya timu ya Louis van Gaal leo yamefungwa na Angel di Maria, Ander Herrera na Juan Mata. Rooney sasa anashika nafasi ya tatu kwa pamoja na Henry katika orodha ya wachezaji waliofunga mabao mengi Ligi Kuu ya England kihistoria, nyuma ya Alan Shearer mwenye mabao 260 na Andrew Cole 187.

Wayne Rooney akishangilia na wachezaji wenzake baada ya kufunga dhidi ya Queens Park Rangers leo
The Manchester United captain scored in the 44th minute to put his side 3-0 up against QPR
Nahodha huyo wa Manchester United akifunga dakika ya 44

WAFUNGAJI BORA WA KIHISTORIA LIGI KUU ENGLAND

1. Alan Shearer - Mabao 260
2. Andrew Cole - Mabao 187 
3 = Thierry Henry - Mabao 175 
3 = Wayne Rooney - Mabao 175 
5. Frank Lampard - Mabao 171
6. Robbie Fowler - Mabao 162 
7. Michael Owen - Mabao 150 
8. Les Ferdinand - Mabao 149 
9. Teddy Sheringham - Mabao 147
10. Robin van Persie - Mabao 134
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
LIKE PAGE YETU HAPO PIA SHARE STORY NA RAFIKI ZAKO

0 comments:

Post a Comment

BURUDANI

 
Top