Kwa mujibu
wa chanzo makini, bosi huyo alitakiwa ajiuzulu mwenyewe katika mkutano
wa wanachama uliofanyika Ijumaa iliyopita katika Viwanja vya Leaders
Club, kutokana na tuhuma mbalimbali huku wanaodaiwa kutangaza nia ya
kugombea urais 2015, Edward Lowassa na Bernard Membe wakitajwa.
Mapaparazi wetu waliokuwepo eneo la tukio, walishuhudia wasanii mbalimbali wakiendesha ajenda ya kumng’oa Steve Nyerere.
Mapaparazi wetu waliokuwepo eneo la tukio, walishuhudia wasanii mbalimbali wakiendesha ajenda ya kumng’oa Steve Nyerere.
Wanachama
hao walidai kwenye uongozi wa Steve kumekuwepo na ufisadi, kutumia
madaraka vibaya na ubadhirifu mkubwa hivyo bora ajiengue. Steve
alionesha kukasirishwa na tuhuma hizo ambazo alidai hazikuwa na ukweli
wowote lakini hadi mwisho wa kikao, wanachama waliendelea kushikilia
msimamo wao kwamba ajiuzulu.
Punde tu
baada ya kikao hicho kilichokosa muafaka kumalizika, Steve Nyerere
alitangaza kupitia mtandao wa Instagram kwamba amejiuzulu wadhifa
wake.Mapaparazi wetu walipomtafuta Steve alifunguka kuwa aliamua
kujiachia ngazi ili kulinda heshima yake.
Hata
hivyo, madai ya Steve Nyerere kujiuzulu yalipingwa vikali na wanachama
wenzake wa Bongo Muvi waliodai kuwa amejikosha lakini ukweli ni kwamba
wamemng’oa.Uongozi wa Steve Nyerere ulioteuliwa mwaka jana, umekuwa
ukikumbwa na kashfa kibao za uchakuchuaji wa fedha zikiwemo za
rambirambi na mambo mengine yahusuyo klabu.
Hata
hivyo, kuna tetesi kwamba wanasiasa wanaotajwa kuwania urais 2015,
Lowassa na Membe ndiyo waliosababisha mtafaruku huo kwa kuwagawa wasanii
hao, kila mmoja akimshabikia mwanasiasa anayemtak
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment