Cristiano Ronaldo atahitaji kulipwa mshahara wa paundi laki 500,000 kwa wiki
CRISTIANO Ronaldo atahitaji kulipwa
mshahara utakaovunja rekodi ya dunia wa paundi 500,000 kwa wiki ili
kujiunga na Chelsea au Manchester United majira ya kiangazi mwakani.
Mwanasoka huyo bora wa dunia na Ulaya,
mnamo mwaka 2013 alionesha nia ya kutaka kurudi United, lakini dili hilo
lilikufa baada ya kuondoka kwa Sir Alex Ferguson.
Hata hivyo United hawakujiandaa kumlipa
Ronaldo anachotaka na aliongeza mkataba na Real Madrid ambapo analipwa
paundi 350,000 kwa wiki.
Atarudi?: Cristiano Ronaldo alifunga goli kwa penalti katika kipigo cha 2-1 kutoka kwa Atletico Madrid jana usiku
Tangu Ronaldo aondoke, United inamlipa
Wayne Rooney paundi 300,000 kwa wiki katika mkataba wake na wiki
iliyopita, Radamel Falcao alisaini mkataba na atalipwa paundi 390,000.
Dili la Falcao lilisainiwa chini ya wakali mkubwa, Jorge Mendes ambaye pia ni wakala wa Ronaldo.
Wamiliki wa kimarekani wa United wamejiandaa kutumia fedha nyingi kumshawishi Ronaldo ili arudi Old Trafford.
Kiukweli, wiki iliyopita, Ronaldo
aliweka wazi kuwa anaweza kuondoka Real Madrid na yuko tayari kurudi
katika klabu yake ya zamani ya United ambapo alikuwa na nia ya kufanya
hivyo mwaka 2013, lakini ilishindikana kutokana na mshahara wake kuwa
mkubwa.
Lakini kutokana na uhusiano wa wakala
Mendes na kocha wa Chelsea, Jose Mourinho na mmiliki, Roman Abramovich,
Ronaldo anaweza kushawishika kujiunga na klabu hiyo ya London Magharibi.
Radamel Falcao analipwa paundi 390,000 kwa katika klabu yake ya Manchester United baada ya kujiunga akitokea Monaco
0 comments:
Post a Comment