“UTAN’TAMBUAJE
kama nimeokooka, utantambuaje kama namuheshimu Mungu…”
Wimbo huu wa Injili ulioimbwa na Bony Mwaitege wengi hupenda
kuusikiliza kama burudani lakini una ujumbe mzito hasa kwa wale
wanaosema wameokoka.
Wanakwaya wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God, Hanipher na Godfrey (mtoto wa mchungaji) walionaswa wakiwa kichakani.
Hivi karibuni mjini Iringa, wanakwaya wawili wa Kanisa la Tanzania
Assemblies of God, mwanamke alijitambulisha kwa jina moja la Hanipher na
mwanaume aliyesema anaitwa Godfrey, walinaswa usiku kichakani katika
mazingira yaliyojaa utata, Risasi Jumamosi linakupa kisa kamili.
NI MAKABURINITukio hilo la kushangaza, lilijiri kwenye eneo la Makanyagio ambalo lina makaburi ya awali katika Manispaa ya Iringa licha ya kuwepo na nyumba za wenyeji pia.
KAZI YA SUNGUSUNGU
Kwa mujibu wa chanzo chetu, wanakwaya hao walinaswa na sungusungu ambao siku za hivi karibuni wamekuwa wakifanya ‘patroo’ katika eneo hilo na la Isoka kufuatia kuwepo kwa matukio ya wakazi wake kuvamiwa, kupigwa na kuporwa mali.
SIKU YA TUKIO
Siku ya tukio, sungusungu hao wakiwa katika majukumu yao waliwaona wanakwaya hao wakiacha njia kuu na kuchepukia porini umbali unaokadiriwa kuwa mita 20 kutoka barabarani.
“Ilibidi sungusungu wawafuate hadi kule kichakani, ndipo walipowakuta katika mazingira tata na yenye maswali mengi bila majibu. Mbaya zaidi, yule mwanamke alikuwa na mtoto wa mwaka mmoja mgongoni,” kilisema chanzo chetu.
Wanakwaya wakifunguka kueleza kisa cha kuwa kichakani usiku mnene.
WAPEWA KICHAPO, WAJIANIKAChanzo kikadai kuwa, sungusungu hao waliwapa kichapo chepesi ili waweze kusema walikuwa wakifanya nini na wao ni akina nani, ndipo mwanamke huyo akaweka wazi mambo kwamba, yeye ni mkazi wa Kitongoji cha Isoka ilhali kijana huyo ni mwimbaji mwenzake wa kwaya lakini pia ni mtoto wa mchungaji wa kanisa hilo.
ETI?
Katika hali ya kushangaza, mtoto huyo wa mchungaji huku akiomba samahani kwa kunaswa kichakani, alisema eti kilichowapeleka huko muda huo wa usiku ni kumsaidia mwanamke huyo kumwingizia nyimbo za dini kwenye simu yake!!
AKIRI SI MWENENDO MWEMA
Pamoja na yote, Godfrey alikiri kuwa kitendo cha kuingia kichakani na mwanamke muda huo wa saa 2.15 usiku kilikuwa ni hatari kwao kiimani na hata usalama wa miili yao kwa ujumla.
Kiimani alikuwa na maana kwamba, kuonekana kichakani watu waliookoka hakutoi picha nzuri kwa jamii inayotakiwa kuhubiriwa ili watu wamrudie Mungu, usalama wa miili ni kama vile kuumwa na nyoka au wadudu wengine wenye kudhuru TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment