Freeman Mbowe, Mwenyekiti Taifa
Profesa Abdallah Safari, Makamu Mwenyekiti (Taifa) Bara
Said Issa Mohamed, Makamu Mwenyekiti (Taifa) Zanzibar
Pascal Katambi Patrobas, Mwenyekiti Bavicha
 Halima James Mdee, Mwenyekiti Bawacha
Hashim Juma Issa, Mwenyekiti Baraza la Wazee
Safu mpya ya uongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) imepatikana baada ya uchaguzi wa Mwenyekiti na makamu wake kumalizika kwa amani jana pale Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
Pengine kilichosalia sasa ni kuona kazi ya kukijenga chama kwa maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa Desemba 14, 2014 pamoja na Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2015.
Kinachotakiwa sasa ni kwa uongozi huo kuweka mikakati ya kujenga chama hicho hadi vijijini, ambako kwa muda mrefu wameshindwa kupata nguvu ya kutosha na kufanya chama tawala CCM kijiimarishe. Vijijini ndiko kwenye wananchi wengi (80% ya Watanzania wako huko) na wanakabiliwa na changamoto nyingi za maisha na kiuchumi.
Freeman Mbowe ameendelea kukalia kiti cha uenyekiti kwa awamu ya tatu sasa baada ya jana kumshinda mpinzani wake pekee Gambaranyera Mong'ateko aliyeambulia kura 20 huku Mbowe akizoa kura 789.
Said Issa Mohamed ametetea nafasi yake ya Makamu Mwenyekiti Zanzibar baada ya kuzoa kura 645 dhidi ya kura 163 za mpinzani wake Hamad Mussa Yusuph.
Naye Profesa Abdallah Safari, ambaye hakuwa na mpinzani, alichaguliwa Makamu Mwenyekiti Bara kwa kuzoa kura za ndiyo 775 huku kura 34 zikimkataa na mbili kuharibika.
Sasa imebaki nafasi ya Katibu Mkuu, ambapo vikao husika vitapanga na kumtangaza kwa mujibu wa taratibu na katiba ya chama hicho.
Awali Chadema ilikwishawapata wenyeviti na wajumbe wa mabaraza mbalimbali katika chaguzi zilizofanyika wiki iliyopita.
Katika Baraza la Wazee, Hashim Juma Issa, alichaguliwa mwenyekiti huku makamu wake kwa Bara akiwa Suzan Lyimo na kwa Zanzibar ni Omar Masoud Omar. Katibu wa Baraza hilo ni Rodrick Emmanuel Lutembeka, mweka hazina ni Erasto Singira Gwita, wakati wajumbe wa baraza kutoka Bara ni Victor Kimesera, Alfred Ntupwa, Florence Kasilima, Hugo Kimaryo, na kutoka Zanzibar ni Hashim Juma Issa.
Wajumbe wa mkutano mkuu waliochaguliwa katika Baraza la Wazee kutoka Bara ni Charles Kikomingo, Mary Nakoe, Mary Joachim, Sylvester Shirima, Timoth Kirway na William Mwangwa, na kutoka Zanzibar ni Rabia Omar, Haji Kali Haji, Khatibu Ally Khatibu na Hassan Herry.
Kwenye Baraza la Vijana, Mwenyekiti mpya ni Pascal Katambi Patribas na makamu wake Bara ni Patrick ole Sosopi na wa Zanzibar ni Zeudi Abdallah, wakati wajumbe wa Baraza Kuu kwa upande wa Bara ni Pasquina Ferdinand Lucas, Pamela Simon Maasay, Joseph Loth Kasambala na Hellen Nagusu Dalali.
Katika Baraza la Wanawake, mwenyekiti mpya ni Halima James Mdee, makamu wake kwa Bara ni Hawa Mwaifunga na kwa Zanzibar ni Hamida Abdallah, wakati wajumbe wa Baraza Kuu kwa upande wa Bara ni Janeth J. Mjungu, Restuta Said Mjoka, Marietha Cosmas Chenyenge na Suzan Hashim Kiwanga, wakati kwa Zanzibar ni Janeth Medadi Fusi.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
LIKE PAGE YETU HAPO PIA SHARE STORY NA RAFIKI ZAKO

0 comments:

Post a Comment

BURUDANI

 
Top