Basi likiwa kwenye mizani baada ya kushusha abiria waliozidisha uzito.
WAKATI serikali ya awamu ya nne inayoongozwa na Rais Jakaya Kikwete
‘JK’ ikifanya kazi nzito ya kujenga barabara kwa gharama kubwa na
kuzilinda kwa kuweka mizani ili kudhibiti magari yanayozidisha uzito, baadhi ya madereva wa mabasi wamekuwa wakikaidi kwa makusudi agizo hilo.
Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’, umebaini
kuwa, baadhi ya madereva wa mabasi hayo wamekuwa wakimpiga changa la
macho Waziri wa Ujenzi, John Magufuli anayesimamia barabara
nchini.Madereva hao huzidisha abiria na hivyo basi kukosa sifa kwenye
mizani wakati wa ukaguzi lakini wanachofanya sasa, kila wanapokaribia
mizani hupunguza uzito kwa kuwashusha baadhi ya abiria nyuma ya mizani
na baadaye kuwapakia kwa mbele baada ya kupima.
Abilia wakipanda baada ya basi kupimwa uzito kwenye mizani. Mwandishi wetu alipokea
taarifa toka kwa wananchi wema wanaolitakia maendeleo taifa lao ambapo
mwishoni mwa wiki iliyopita, paparazi wetu alifanya uchungu na kubaini
uwepo wa hujuma hizo za makusudi.
Basi moja linalofanya safari zake kati ya Moshi (Kilimanjaro) na Dar
es Salaam (jina tunalo) lilinaswa likifanya mchezo huo kwenye mizani
iliyopo jirani na Daraja la Wami.
Mbunge wa jimbo la Chato na waziri wa Ujenzi Mhe. Dk. John Pombe
Magufuli Dereva wa basi hilo aliwashusha abiria zaidi ya watano ambao
walitembea kwa miguu hadi ng’ambo ya pili ya mizani hiyo na baada ya
basi hilo kupima uzito, kondakta aliwaita abiria hao kama anavyoonekana pichani na kuwapakia tena.
Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli alipotafutwa na mwandishi wetu
kuhusiana na tukio hilo, simu yake haikupatikana. Jitihada zinaendelea
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment