Siku
moja baada ya shirikisho la sokanchini TFF kumtangaza mchezaji Emmanuel
Okwi kuwa huru na hivyo anaweza kusajiliwa na klabu ya Simba – leo hii
uongozi wa klabu ya Yanga umeitisha mkutano wa waandishi wa habari na
kuzungumza juu ya uamuzi wa keshi yao dhidi ya Okwi.Uongozi wa Yanga
umesema utapinga maamuzi ya kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji
kuhusiana na maamuzi yake ya kumtangaza mchezaji wake, Emmanuel Okwi
kuwa huru.Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria ya Yanga, Sam Mapande amesema
kuwa hawajaridhishwa na maamuzi hayo ambayo yanakinzana na shitaka zima
la mchezaji huyo.Mapande amesema kuwa kamati ya TFF imeamua sakata la
Okwi kinyume na malalamiko yao kwani hakukuwa na lalamiko la mchezaji
huyo wa Uganda kuhusiana na malipo ya fedha zake za usajili.Alisema kuwa
cha kushangaza, kamati hiyo ya TFF iliamua kusikiliza kesi ambayo
haikuwa mbele yao na kutoa maamuzi ambayo hata wao wameshangazwa
nayo.“Kwanza kesi yenyewe ilikuwa haijamalizika, walituambia tuwasilishe
vielelezo kuhusiana na kitendo cha mchezaji huyo kufanya mazungumzo na
klabu ya Misri, lakinicha kushangaza maamuzi yametolewa, hili
limetushangaza sana,” alisema Mapande.Alisema kuwa mazingira yalikuwa
yameandaliwa kuibeba Simba na Okwi kwani hata malalamiko yao kwa Simba
hayakusikilizwa. “Malalamiko yetu yalikuwa wazi kabisa, yapo
kimaandishi, hatukuwai kulalamikiwa, suala la fedha za usajilila Okwi
limetoka wapi, kama lilikuwepo, mbona hatujajulishwa kimaandishi kama
utaratibu ulivyo,” alisema.Alisema kuwa Kamati hiyo kumruhusu mmoja wa
wajumbe wa kamati hiyo Zacharia Hans Pope ambaye pia ni mwenyekiti
wakamati ya usajili ya Simba kuwemo katika kikao hicho kinyume na
taratibu za Fifa kupitia kifungu namba 19 kinachoeleza mgongano wa
kimaslah
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
LIKE PAGE YETU HAPO PIA SHARE STORY NA RAFIKI ZAKO
0 comments:
Post a Comment