Mwanafunzi
wa Chuo cha Uuguzi Chimala wilayani Mbarali, Mkoa wa Mbeya, Vena Mtati
(27) (pichani) anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa kwa madai
mazito ya kumuua mtoto wake kwa kumnyonga, kumtumbukiza kwenye mfuko wa
rambo na kuutia ndani ya mfuko wa salfeti kisha kuuficha chini ya
kitanda.
Tukio
hilo la kikatili ambalo limewashangaza wengi, hasa ikizingatiwa kuwa
mtuhumiwa huyo anajua sheria kwa sababu anajifunza uuguzi, lilijiri
Agosti 21, mwaka huu ndani ya nyumba moja iliyopo Kijiweni, Kata ya
Mvinjeni mjini hapa.
Kwa
mujibu wa shuhuda ambaye anaishi jirani na nyumba inayodaiwa kufanyika
mauaji hayo (jina lipo), wiki mbili zilizopita, mtuhumiwa huyo alifika
kwenye nyumba hiyo akitokea chuoni akiwa na ujauzito.
“Wiki
mbili zilizopita, Vena alifikia kwa rafiki yake anayeitwa Joyce ambaye
alikuwa amepangisha katika hiyo nyumba. Vena alikuwa na mimba kubwa,
baada ya siku tano tu akajifungua,” kilisema chanzo hicho.
Kikaongeza: “Siku
ya tukio, Joyce yeye ambaye ni mwenyeji alitoka kwenda katika shughuli
zake, akamuacha Vena akiwa chumbani. Nadhani ndipo aliposhikwa na
uchungu, akajifugua mtoto wa kike.
“Ilikuwa
asubuhi, sisi tukasikia kelele kutoka kwenye chumba hicho. Zile kelele
zilikuwa si za kawaida! Ilikuwa kama vile kuna mtu anakabwa.
“Tuliposikiliza
kwa makini, mara sauti ya redio ikaongezwa ili kufanya kelele hizo
zisisikike kwa nje. Lakini kwa vile sisi majirani tulijua kwamba ndani
ya chumba kile kuna mjamzito na kelele alizopiga mtoto si za kawaida
ndipo tulipomtafuta mwandishi wa habari (hizi),” kilisema chanzo hicho.
Mwandishi
wetu alipopatikana na kunyetishiwa kuhusu kuwepo kwa uwezekano wa mama
ambaye ni nesi kumuua mtoto wake aliyejifungua, aliwasiliana na Polisi
wa Dawati la Jinsia.
Denti (aliyeshika kiroba chenye mwili) akiwa chini ya ulinzi wa polisi (Kulia) ni mwenyeji wake, Joyce.
Polisi hao, awali walimtafuta mwenyeji wa mtuhumiwa huyo, yaani Joyce ambaye alikuwa kwenye mihangaiko yake.
Alipopatikana alipokonywa simu yake ya mkononi ili asiweze kuwasiliana na mtuhumiwa.
Aliulizwa
kama ana mgeni nyumbani kwake, akakiri. Akaulizwa kama mgeni huyo
amejifungua, akakataa ndipo wakamchukua kwenda naye nyumbani kwake
kumfuata mtuhumiwa huyo.
Mwandishi wetu akiwa ameongozana na askari hao walifika kwenye chumba hicho na kumkuta Vena akiwa amesimama mlangoni.
Alipoulizwa
kama amejifungua, awali alikataa katakata lakini baada ya kubanwa na
kutishiwa kuswekwa ndani, alikiri kujifungua na kusema kwamba mtoto huyo
amemficha uvunguni mwa kitanda.
Ndani ya chumba hicho, sakafuni kulikuwa na damu zilizodaiwa kumtoka mtuhumiwa huyo wakati akijifungua mwenyewe!
Polisi
walizama chumbani, wakainama kuchungulia chini ya kitanda. Walichoanza
kukiona ni mfuko wa salfeti, wakauvuta kuutoa. Walipofungua ndani,
wakakuta mfuko wa rambo, wakaingiza mkono na kutoa kifurushi kikiwa
kimeviringishwa nguo nyingi na ndiye mtoto huyo alimohifadhiwa.
Mbali
na mwili wa mtoto huyo kuviringishwa nguo hizo, pia ulimwagiwa chumvi
na vumbi la mkaa ambapo ilidaiwa mtuhumiwa alifanya hivyo ili mwili huo
usitoe harufu utakapotupwa porini.
Majirani
walisema maarifa hayo, mtuhumiwa aliyapata kwa sababu tayari anajua
namna ya kuhifadhi mwili wa mwanadamu, kwa mwanamke asiye na ujuzi
asingeweza kufanya hivyo.
Kuna
madai kwamba, mtuhumiwa huyo aliwaambia polisi kuwa alifikia uamuzi wa
kumuua mtoto huyo kufuatia mwanaume aliyempa ujauzito aishiye jijini Dar
es Salaam kumuahidi ndoa lakini akaingia mitini.
Baada
ya polisi kusikiliza maelezo ya mtuhumiwa huyo, walimkamata yeye,
mwenyeji wake Joyce na mmiliki wa nyumba hiyo ambaye jina halikupatikana
mara moja.
Polisi
walisema mmiliki wa nyumba hiyo alikamatwa kwa sababu alikiuka sheria
za mji ambapo alitakiwa kutoa taarifa za kumpokea mgeni huyo kwenye
serikali za mitaa lakini hakufanya hivyo huku Joyce akidaiwa kutambua
kuwa mgeni wake alijifungua lakini akawaambia hakujifungua.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Ramadhan Mungi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo