IMANI ya kuabudu inayotiliwa shaka duniani ya Freemason imetajwa kuwa nyuma ya pazia la ajali mbaya ya Basi la Sumry iliyotokea katika Kijiji cha Ulyampiti mkoani Singida mwanzoni mwa wiki iliyopita na kusababisha vifo vya watu 19, wakiwemo polisi wa usalama barabarani wanne.
Basi la Sumry lililopata ajali mbaya iliyotokea katika Kijiji cha Ulyampiti mkoani Singida mwanzoni mwa wiki iliyopita.
Habari za uhakika kutoka kijijini hapo zinasema siku moja baada ya ajali hiyo mbaya, basi moja linalosafiri kati ya miji ya Bukoba na Dar es Salaam (jina linahifadhiwa) lilipita katika kijiji hicho na kutupa karatasi zilizokuwa na maneno ya kuwahamasisha watu kujiunga na dini hiyo inayodaiwa kuwa ya kishetani.
Inadaiwa kuwa kwenye karatasi hizo kulikuwa na mchoro unaoaminika kutumiwa na watu wa dini hiyo ambapo pia ilichorwa michoro yenye kuonesha burungutu la fedha, sanjari na namba za simu zinazowataka watu kuzitumia endapo watataka kujiunga.
Baadhi ya watu waliopoteza maisha kutokana na ajali hiyo.
Tulipoziona zile karatasi na kuzisoma, wengi tulikimbia kwa sababu tunahusisha kabisa na ajali ya Sumry. Mbaya zaidi ajali yenyewe inatia shaka. Mimi nilipoambiwa kuhusu hizo karatasi, sikutaka kuziona, nikakimbia,î alisema mwanamke mmoja aliyejitambulisha kwa jina la  Yasinta, mkazi wa kijiji hicho.
Alisema karatasi hizo zilitupwa pia katika Vijiji vya Isuna, Nkuhi, Samumba na Ikungi wakati basi hilo ambalo mara kwa mara huripotiwa kupata ajali, likiwa katika safari yake kuelekea Dar es Salaam.
Kijana mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Zuberi ambaye hufanya shughuli zake katika stendi ya mabasi Kijiji cha Ulyampiti alithibitisha kutupwa kwa karatasi hizo na yeye alikuwa nayo mkononi.
ìNi kweli hizo karatasi zimetupwa, hata washikaji wa vijiji vya jirani nao wametuambia wameokota, mimi mwenyewe hapa nilipo ninayo, ina namba za simu ambazo wanasema tuwasiliane nao kama tunataka kujiunga,î alisema kijana huyo na kutaja namba hizo, ambazo hata hivyo haziwezi kuandikwa gazetini kwa sababu maalum.
Wanakijiji hao walikwenda mbali zaidi na kudai kuwa basi lilitupa karatasi hizo pia limechorwa alama inayodaiwa kutumiwa na watu wa imani hiyo katika moja ya sehemu za gari hilo ambalo hata hivyo, gazeti letu linaendelea kufuatilia kwa karibu sakata hilo ili kujiridhisha.
Ajali ya Basi la Sumry ilitokea Jumatatu iliyopita majira ya usiku, baada ya gari hilo kuacha njia na kulifuata kundi la watu lililokuwa pembeni likishuhudia askari polisi wakiuchukua mwili wa mtu mmoja aliyegongwa na gari akiwa katika pikipiki.
Inadaiwa kuwa kipande ambacho ajali hiyo imetokea kimekuwa na matukio mengi ya kushangaza, kwani mara nyingi zinatokea ajali za kushangaza ambazo katika kipindi cha miaka minne sasa, watu zaidi ya 50 wamepoteza maisha katika maeneo ya jirani ya
vijiji hivyo.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
LIKE PAGE YETU HAPO PIA SHARE STORY NA RAFIKI ZAKO

0 comments:

Post a Comment

BURUDANI

 
Top