Serengeti. Walimu na wanafunzi wa Sekondari ya
Kambarage wilayani hapa wamejikuta katika wakati mgumu kutokana na mmoja
wa wanafunzi kuvamia shule akiwa na silaha za jadi akitishia kuwadhuru
huku ikidaiwa kuwa alikumbwa na pepo.
Katika tukio hilo inadaiwa wanafunzi wawili wa
kike walipoteza fahamu kwa hofu. Tukio hilo linadaiwa kutokea Aprili 23
saa 6:00 mchana na kudumu kwa zaidi ya dakika 25.
Makamu Mkuu wa Shule, Charles Malima alisema akiwa
ofisini ghafla alisikia kelele za walimu wa kike waliokuwa wakisubiri
usafari wakiomba msaada wakiwa wanakimbia huku mwanafunzi akiwafukuza
akiwa ameshika panga.
“Nilidhani wameumwa na nyuki walioko eneo hilo…
Nilipoangalia nikamwona mtu ameshika panga, upinde, mishale miwili na
rungu kiunoni akiwafukuza kwa kasi, wananchi walikuwa nyuma wanakuja
kuwaokoa,” alisema Mwalimu Malima.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment