Bi Cheka akiwa nje ya nyumba
anayoishi.
DAH MASIKINI! Hivi ndivyo unavyoweza
kusema wakati unapomuona msanii wa
muziki wa kizazi kipya, Cheka Hija,
maarufu kama Bi. Cheka kutoka Kundi la
Mkubwa na Wanawe, linaloongozwa na
Said Fella ‘Mkubwa’ lenye maskani yake,
Temeke jijini Dar es Salaam.
Mtoa habari wetu aliwasiliana na gazeti hili
na kulieleza kuwa msanii huyo mwenye
umri wa miaka 55, hivi karibuni alianguka
ghafla nyumbani kwake na kukata kauli,
wakati alipokuwa akienda chooni
kujisaidia.
Wikiendi iliyopita, Amani lilifika nyumbani
kwa msanii huyo mzee, anayeishi Bunju B,
nje kidogo ya jiji la Dar na kumkuta akiwa
na wajukuu zake huku hali yake ikiwa tete
tokea alipoanguka Oktoba mwaka huu .
Akiwa anaishi katika kijumba chake
kilichojengwa kwa miti na kukandikwa
udongo, mtu anayemuona katika luninga
akifanya vitu vyake, asingeweza kuamini
kama hapo ndipo anapoishi.
Upande wa nyumba yake.
“Ukweli nilikuwa na hali mbaya, afadhali
sasa, naongea na kusimama kwani nilikuwa
siwezi kutembea, wiki iliyopita alikuja
meneja wetu, Yusuf Chambuso na akina
Dogo Aslay.
“Jamani maisha yangu kwa sasa ni magumu
kwani siwezi kufanya kazi yoyote na sina
msaada na kwenye muziki sijaona faida
yoyote labda ya nguo tu, kwamba nilizoea
kuvaa madela na kanzu sasa nina suruali,”
alisema Bi Cheka kwa machungu.
Bi Cheka akiwa na wajukuu zake.
Alisema anasikitishwa na maisha yake
kwani kutokana na umaarufu wake, mtaani
kwao anaonekana kama mtu mwenye
uwezo, wakati siyo kweli kwani anaishi
kwenye nyumba ya tembe katikati ya
nyumba nzuri.
“Kuhusu malipo makubwa kuwahi kupata
ni shilingi laki tatu nilizolipwa kwenye shoo
ya Fiesta mwaka juzi, hizo ndizo hela
kubwa niliyowahi kupata katika
muziki.”Gazeti hili lilimtafuta Fella ambaye
alikiri Bi. Cheka kuumwa, akisema
anasumbuliwa na magonjwa ya uzee na
kwamba ahadi yake ya kumsaidia kujenga
nyumba imeishia kwenye mchango wake
wa matofari.
...Bi Cheka akiimba na Chege.
“Mimi kama Fella nimesaidia ninapoweza,
nimemchangia matofari kidogo, kwa hiyo
watanzania wenzangu nao tuungane
tumchangie ili aweze kurekebisha kibanda
chake,” alisem
Global Publishers inaanzisha kampeni
maalum ya kumsaidia na hivyo inawaomba
watanzania kumchangia msanii huyu ili
apate nyumba nzuri na matibabu yake. Ili
kumsaidia tuma fedha kwenye namba
0654-880707 ambayo itasimamiwa na
kampuni.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
LIKE PAGE YETU HAPO PIA SHARE STORY NA RAFIKI ZAKO

0 comments:

Post a Comment

BURUDANI

 
Top