wazo zuri au kubwa la biashara, lakini huo ni
mwanzo tu. Kuna habari za mtaani nyingi sana
ukiona hivyo inawezekana ukafikiri kuwa utakuwa
mtu uliyefanikiwa muda si mrefu sana. Hebu fikiria
kwenye mpango wako na ujaribu kuangalia soko na
maisha yako binafsi. Utahitajika kujua je mteja
wako ni nani na uweze kuweka hiyo biashara ni kitu
cha muhimu kwenye maisha yako. Bila ya kufanya
hivyo uwezekano wa kufanikiwa ni mdogo;
Hebu jiulize maswali yafuatayo na ujue kweli wewe
kama ni mjasiriamali
1. Je unatumia muda wako mwingi kwenye
biashara yako?
Kama unatumia muda mchache kwenye biashara
yako na inakuwa tu kama kamradi ka pembeni
inaweza ikakusumbua kwani muda wako unahitajika
sana. Unatakiwa uweke muda na malengo yako
kwa ujumla kwenye biashara hiyo, inakuwa ngumu
kutegemea biashara yako huku ukitumia muda
mwingi kwenye kazi uliyoajiriwa. Unahitaji kujitoa
kwa moyo wako wote kwenye biashara yako,
inakuhitaji sana ili ikue.
2. Je kuna uhitaji wa bidhaa au huduma?
Unachotakiwa kuangalia je huduma yako au bidhaa
yako ina wahitaji? Je ni kweli kwamba bidhaa au
huduma yako inahitajika? Hata kama kitu
unachouza ni cha tofauti au kinafanana na vingine
lazima uonyeshe utofauti ili uweze kupambana
kwenye soko la ushindani.
3. Je uko tayari kukabiliana na shida?
Unapoanza biashara utakutana na shida na adha
nyingi sana hata kama mpango wako wa biashara
ni mzuri kiasi gani. Ni kitu kimoja kuwa na mpango
mzuri na ni kitu kingine kujua shughuli za kila siku
za hiyo biashara. Unatakiwa kujiandaa kwa mambo
ambayo huyategemei na uwe na uwezo wa
kujikwamua kutokana na hayo.
4. Je unajua kwa uhalisia mapato yako yatatokana
na nini?
Unahitaji mfumo wa biashara, na uweze kujua
wateja wako na unawezaje kutengeneza pesa
baada ya kuwafikia. Kuwa na wazo zuni
hakutaifanya biashara yako kufanikiwa. Unatakiwa
kujua nani anahitaji bidhaa au huduma yako na
uweze kuitathimini jinsi gani itakuwa hela halisi.
5. Je kufanya biashara ni kitu cha msingi na
muhimu kwenye maisha yako?
Mashaka na wasiwasi wa familia unaweza kuharibu
biashara yako, je uko tayari kutumia siku zote za
wiki kufanya kazi bila kujali Jumamosi na Jumapili?
Hakuna namna unaweza kujenga biashara yako bila
kutoa sadaka katika sehemu fulani ya maisha yako.
Kama hauko tayari kufanya hivyo inamaanisha
utakutana na vitu vigumu sana na biashara yako
haitafanikiwa.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
LIKE PAGE YETU HAPO PIA SHARE STORY NA RAFIKI ZAKO

0 comments:

Post a Comment

BURUDANI

 
Top