Mrisho Mpoto ameungana na wasanii wengine 20 barani Afrika kutengeneza wimbo maalum wa kuelimisha jamii kuhusiana na kupambana na ugonjwa wa Ebola. Msanii huyo aliteuliwa na Kora kuwa balozi wa Tanzania na ugonjwa wa Ebola.
Msemaji wa Mpoto Theatre Gallery Ltd, Dominic ameiambia Bongo5 kuwa nafasi aliyoipata Mpoto kufanya kazi na wasanii mbalimbali wa Afrika ni njia moja wapo ya kumtangaza na kuufikisha muziki wake mbali zaidi.“Mpoto ameshaanza kurekodi, pia hao wasanii 20 wa Afrika ambao ni mabalozi wa kupambana na ugonjwa wa Ebola, tayari na wao wameshaanza kurekodi. Kwahiyo ni nyimbo ya pamoja ambayo inazungumzia kupiga vita maambukizi ya Ebola. Hii project ipo chini ya Kora, mpaka sasa hivi maandalizi yapo vizuri na soon watanzania na waafrika kwa ujumla wataanza kusikia project hiyo,” amesema Dominic. TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment