Rais wa Burkina Faso Blaise Compaire ametangaza kujiuzulu, kufuatia maandamano yenye ghasia wakati akijaribu kuongeza utawala wake wa miaka 27.
Compaire alitoa maelezo yanayosema nafasi ya urais ipo na kuahidi uchaguzi ndani ya siku 90.
Mkuu wa jeshi Jenerali Honore Traore alisema amechukua madaraka ya taifa hilo “kwa mujibu ya vifungu vya katiba”.
Halaiki ya watu walicheza na kufurahi katika mji mkuu, Ouagadougou, baada ya kujizulu kwa Compaire kutangazwa.
Siku ya Alhamisi, waandamanaji wenye hasira walilichoma moto bunge na majengo ya serikali baada ya serikali kutaka kubadili katiba.
0 comments:
Post a Comment