Manchester
United imejikuta ikiindelea kuwa wanyonge wa Manchester City baada ya
kukubali kipigo cha 1-0 katika mchezo mkali uliofanyika katika uwanja wa
Etihad, Jumapili, goli lililofungwa na Sergio Aguero dakika ya 63.
Kocha
wa Manchester United, Louis van Gaal amemlaumu beki wake Chris Smalling
kwa kitendo cha kutolewa akidai kilikuwa cha ‘kijinga’.
Smalling
alitolewa kabla ya mapumziko kwa kupewa kadi mbili ya kwanza kwa kuzuia
mpira wa mlinda mlango wa Man City, Joe Hart, ya pili ni kwa kumkaba
vibaya James Milner. “Kwenye mechi kama ya dabi lazima uwe makini kadi
ya pili ya njano ilikuwa ya kijinga, “ Van Gaal aliiambia BBC Sport.
Kwa upande mwingine Van Gaal alitokea kumtetea Marouanne Fellaini baada ya kiungo huyo kuonekana akimtemea mate Sergio Aguero.
“Televisheni
ilimuonyesha akipiga kelele, na wakati mwingine ukipiga kelele unaweza
kutokwa na mate kidogo” alisema kocha huyo lakini picha zinaonyesha
Fellaini raia wa Ubelgiji akimtemea mate Aguero wakati akimlaumu kuwa
alijiangusha.
Lakini picha zimebadili mchezo huo na huenda Mbelgiji huyo mwenye asili ya kiarabu akakumbana na adhabu ya FA.
Bonyezahapa
0 comments:
Post a Comment