Nyota wa sinema Bongo, Aunty Ezekiel akiwa Bongo.
Stori: Mayasa Mariwata na Shani Ramadhani NYOTA wa
sinema Bongo, Aunty Ezekiel ameingia matatani na maafande wa Kituo cha
Polisi Pangani, Ilala jijini Dar akidaiwa kutokomea na cheni ya Shabani
Limo yenye thamani ya shilingi milioni 6.
Kwa
mujibu wa chanzo, mwishoni mwa Februari, mwaka huu, Aunty alikwenda kwa
Shabani na kuazima cheni hiyo kwa makubaliano ya kuirejesha baada ya
muda jambo ambalo hakulifanya na baadaye, Septemba mwaka huu, akasafiri
kwenda Marekani kutangaza utalii wa ndani.
Baada ya kurejea, Oktoba mwaka huu, Shabani alimkomalia Aunty na kufikishana Kituo cha Polisi Oysterbay, Dar ambapo staa huyo alisema na yeye alimwazima cheni hiyo rafiki yake aitwaye Neema.
Ilidaiwa kuwa, Neema baada ya kubanwa alikiri na kusema aliiweka bondi cheni hiyo na hapo ndipo danadana zilipoanza hivyo jamaa akaamua kwenda kufungua madai mengine Kituo cha Polisi Pangani.
Jumatano iliyopita, mapaparazi wetu walifunga safari mpaka kituoni hapo ambapo baadhi ya askari walikiri kuwepo kwa kesi hiyo lakini waligoma kutoa namba za kumbukumbu za jalada ‘RB’ wakidai mwenye uwezo huo ni Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova.

Aunty Ezekiel akiwa Marekani alipokwenda kutangaza utalii wa ndani.
“Ni
kweli hapa kuna hiyo kesi na ilianzia Oysterbay japo hatuwezi kuitolea
maelezo ya kina kwa vile jambo lenyewe limekaa kimapenzi zaidi,” alisema
askari mmoja ambaye hakuwa tayari kutaja jina lake.
Shabani alipotafutwa kwa njia ya simu na kuulizwa juu ya taarifa hizo alisema alimuazima Aunty cheni hiyo ambapo naye alimpa shoga yake.
Aunty alipopatikana na kuulizwa alikana kumfahamu Shabani na kudai hana taarifa zozote za kuwepo kwa ishu hiyo.“Mh! Huo ni uzushi, hakuna kitu kama hicho na wala hizo taarifa sizifahamu, huyo mwanaume simjui ndiyo kwanza namsikia kwako,”alisema Aunty.

0 comments:
Post a Comment