Wakati Rais wa jamuhuri ya muungano wa
Tanzania Dk Jakaya Mrisho Kikwete akitarajiwa kukabidhiwa rasimu ya
katiba iliyopendekezwa na Bunge maalum kesho mjini Dodoma maandalizi
kabambe kwa ajili ya hafla hiyo yanafanyika mjini humo huku idadi kubwa
ya wageni wakiwasili ambapo hali ya ulinzi imeimarishwa mara dufu
kuelekea katika tukio hilo la kihistoria.
Hii ndio mandhari ya mji wa Dodoma katika kuelekea siku hii muhimu
katika historia ya Tanzania ambapo kamera ya ITV imeshuhudia watu kwa
makundi kutoka nje ya mji wa Dodoma yakiwasili huku katika eneo la
uwanja wa jamuhuri ambako tukio hilo litafanyika umepambwa kwa majukwa
na nakshi za aina mbalimbali sambamba na kufanyika kwa usafi na ulinzi
wa hali ya juu.
Zaidi ya wageni 3000 wakiwemo viongozi wa kitaifa na makundi mbalimbali
ya kijamii kutoka mikoa yote ya Tanzania bara na Zanzibar wanatarajiwa
kushuhudia tukio hilo la kihistoria ambapo jeshi la polisi mkoa wa
Dodoma kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama
wameimarisha ulinzi mara dufu katika viunga vya mji wa Dodoma ili
kuhakikisha hali ya ulinzi inaboreka wakati wote kabla wakati na baada
ya tukio hilo adhimu.
Mbali na rais Kikwete ambaye ataongoza shughuli hiyo pia atakuwepo rais
wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar pamoja makamu wa rais wote wa
muungano na Zanzibar, waziri mkuu, waziri kiongozi na mawaziri wakuu na
viongozi wote wastaafu wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania mabalozi wa
nchi mbalimbali na wawakilishi wa jumuiya za kimataifa.
Wakati huohuo mkoa wa Dodoma umefanya dua maalum ya kuliombea taifa amani katika kuelekea sh
ughuli hiyo ambapo viongozi wa dini ya madhehebu mbalimbali wameongoza
dua hiyo iliyofanyika katika viwanja vya Nyerere vilivyoko katikati ya
mji wa Dodoma
0 comments:
Post a Comment