Familia ya Mwathiriwa wa kwanza wa Ugonjwa huo iliwinda Popo ambao huwa na virusi vya Ebola.
Lakini katika baadhi ya wanyama hawa huwa wamebeba magonjwa hatari.
Kama
Popo huwa wamebeba virusi aina tofauti ambavyo ni hatari kwa mwili wa
binadamu huku baadhi ya Popo wanaokula matunda wakiwa na virusi vya
Ebola.
Kinyesi cha wanyama hao kilicho na virusi hivyo kinaweza kuwaathri wanyama wengine kama vile Nyani na Sokwe.
Kwa wanyama hao kama kwa binadamu virusi hivyo vinaweza kuwa hatari.
Lakini Popo wanaweza wasiathirike sana.
Kwa hivyo inakuwa rahisi kwao kubeba virusi hivyo bila ya kuathirika kwa vyovyote.
Je
ulaji wa nyama ya wanyama wa msituni inaweza kuwa ndio chanzo cha janga
la Ebola ambalo limekumba hasa kanda ya Afriak Magharibi?
Kitovu
cha janga hilo kimesemekana kuwa mtoto mwenye umri wa miaka miwili
kutoka kijiji cha Gueckedou Kusini Mashariki mwa Guinea, eneo ambalo
nyama Popo ambayo huwindwa na kuliwa mara kwa mara.
Mtoto huyo aliyesemekana kuitwa, Child Zero, alifariki tarehe sita Disemba mwaka 2013.
Hata
hivyo haijulikani ambavyo virusi hivyo vinaathiri mwili wa binadamu,
kulingana na Profesa Jonathan Ball,mtaalamu wa virusi katika chuo kikuu
cha Nottingham.
Nyama hiyo huuzwa katika masoko mengi katika eneo hilo
Anasema
inawezekana virusi hivyo hupitia kwa wanyama kama Nyani lakini ushahidi
unaonyesha kuwa virusi hivyo pia vinaweza kupitia kwa Popo.
Hata hivyo anasema ni vigumu kwa virusi kutoka kwa mnyama hadi kwa binadamu.
Anasema mwanzo virusi vinaingia kwa seli za mwili ambapo vinazaana kwa kuugusana na damu mwilini.
Familia ya mtoto huyo,ilisema kuwa iliwinda aina mbili ya Popo ambayo huwa na virusi vya Ebola.
Nyama ya msituni inaweza kutoka kwa Nyani, Popo wanaokula matunda na wakati mwingine hata kutoka kwa Panya na Nyoka.
Kutoka
katika maeneo mengine nyama hii huwa ni mlo muhimu kwa jamii lakini kwa
wengine hula tu kama njia ya kufurahisha nafsi zao.
Nchini
DRC watu hula milioni ya tani za nyama ya wanyama wa msituni kwa mujibu
wa shirika la utafiti la (Centre of International Forestry Research,)
kila mwaka.
Sio nchini DRC pekee ambako nyama ya wanyama wa msituni huliwa bali pia nchini Ghana.
Lakini cha kushangaza ni kwamba hapajakuwa na hata kisa kimoja cha maambukizi ya Ebola nchini Ghana.
0 comments:
Post a Comment