Watu nane walichapwa bakora mbele ya watu 1,000 ndani ya msikiti nchini
Indonesia baada ya kuvunja sheria ya Kiislamu kwa kucheza kamari.
Mwendesha mashtaka wa nchi, kwenye jimbo la Aceh, kaskazini-magharibi
mwa Sumatra, alisoma adhabu hiyo mbele ya mtu aliyejifichwa uso akiwa
amevaa nguo ndefu ya hudhurungi.
Akitumia fimbo nyembamba ya mti wa mpingo, aliwachapa kwenye makalio watu hao fimbo tano kila mmoja.
Msikiti ulijawa na watu wakati wa adhabu hiyo iliyofuatiwa na ibada ya Ijumaa asubuhi.
Adhabu hiyo ya fimbo ilifuatia baada ya kukamatwa watu tisa kwa kucheza
kamari mwezi Julai. Polisi walikamata kisasi cha pauni 80 (208,000)
kutoka kwa watu hao.
Mmoja wao hakuweza kuchapwa kwa sababu ya afya yake ila atakabiliana na
adhabu hiyo atakapopona, alisema mwendesha mashtaka wa nchi Nurhalma
ambaye anatumia jina moja tu.
0 comments:
Post a Comment