Hatimaye yule mwanaume aliyedaiwa kufumaniwa na mke wa mtu na hatimaye
kufanyiwa usodoma na watu sita, akiwemo mume wa mwanamke huyo
amefungukia mchezo mzima.
Hivi karibuni mwanaume huyo (jina tunalo) ambaye ni mume wa wake
wawili na mkazi wa Yombo Kiwalani, Wilaya ya Ilala jijini Dar mwenye
umri wa miaka 34 alikutwa na mkasa huo kwenye nyumba ya kulala wageni
iitwayo Yombo Executive inayomilikiwa na Athuman Maembe.
Mara baada ya picha za tukio hilo kuenea kwenye mitandao ya kijamii
na watu kushangaa, gazeti hili lilituma timu yake ya habari za uchunguzi
ili kupata ukweli wa tukio hilo.Uwazi lilifanikiwa kumpata mwanamume
huyo ambaye ni mfanyabiashara, pia alijitambulisha kuwa yeye ni
mwelimishaji rika wa magonjwa ya ngono, afya ya uzazi, madawa ya kulevya
na unyanyasaji wa kijinsia.
Alianza kwa kusema: “Ni kweli mimi ndiye niliyetendewa ukatili ule.
Natamani kujiua kwani mambo yale nayasikia tu usiombe yakukute.
“Nimefedheheka sana, sina mahala pa kuficha aibu hii kubwa. Kila
nikikumbuka kuwa nina wake wawili na watoto, wazazi, marafiki na ndugu,
bora hata wangeniua kuliko kuniacha nazidi kudhalilika hivi.
“Siku ya tukio ilikuwa Jumamosi ya Agosti 23, mwaka huu. Kuna mwanamke mmoja anaitwa mama Lilly alinipigia simu. Kwanza alikuwa akinipigia simu mara kwa mara wiki moja kabla ya tukio akinieleza kwamba ana shida na mimi, alisema mume wake amekuwa akimnyanyasa kijinsia.
“Siku hiyo, saa tatu asubuhi mama Lilly alinipigia simu huku analia,
akasema kwamba mumewe kampiga na kumfukuza nyumbani hivyo anaomba
kuonana na mimi kwa ajili ya ushauri ila alitaka tukutane naye maeneo ya
Mtongani, Mbagala au Tandika.
“Nilikataa, nikamwambia aje kwenye Ukumbi wa Maembe ninakotoaga
mafunzo mbalimbali kwa vijana. Ukumbi huo upo karibu na nyumba hiyo ya
kulala wageni kulikotokea tukio.
“Huyu mwanamke namfahamu kwani kipindi cha nyuma alikuwa na stationary karibu na maeneo haya, nilikuwa nikimtengenezea kompyuta lakini miaka miwili iliyopita alihama na sikujua alipo hadi hivi karibuni aliponipigia simu.
“Huyu mwanamke namfahamu kwani kipindi cha nyuma alikuwa na stationary karibu na maeneo haya, nilikuwa nikimtengenezea kompyuta lakini miaka miwili iliyopita alihama na sikujua alipo hadi hivi karibuni aliponipigia simu.
“Basi, nilipomwambia aje yeye maeneo haya, aliamua kunifuata. Alifika
saa saba mchana huku akibubujikwa machozi, nilimsikiliza kwa makini
matatizo yake mwishowe aliniomba nimkopeshe shilingi laki moja ili aende
kwao, nilimjibu kwa pale sikuwa nazo labda mpaka Jumatatu.
“Akasema kama ni hivyo basi nimsaidie sehemu ya kulala ili kesho yake
aondoke kwenda kwa dada yake. Nilimuonea huruma, nilimchukulia chumba,
nikamwambia kama kutakuwa na tatizo anipigie simu. Wakati najiandaa
kutoka chumbani aliendelea kuongea maneno mengi sana ya kunifanya
niendelee kuwepo.
“Wakati huo alikuwa akituma ujumbe wa simu sehemu nisiyoijua. Sasa
nilipoagana naye, ile natoka tu, mlangoni niliona wanaume sita
wakanirudisha chumbani na kufunga mlango.“Wakaniambia niwape namba yangu
ya akaunti ya benki na password ya simu yangu kwani walijua kwamba
tayari nimetumiwa fedha kutoka nje ya nchi kutoka kwa wafadhili.
“Niliwaambia sina akaunti, wakanipiga sana, ikabidi niwaongopee
kwamba nyumbani nina shilingi laki tano, wakaniambia niwaelekeze
nyumbani, nikafanya hivyo. Wawili kati yao waliondoka na pikipiki hadi
kwangu kuchukua fedha, wengine wakawa wamenizuia chumbani na kunitishia
nikipiga kelele ndiyo mwisho wa maisha yangu.
“Wale walipofika kwangu walimwambia mke wangu awape laki tano na
walimtaka aongee na mimi kwa simu huku nikiwa chini ya ulinzi. Mke wangu
aliwaambia hana fedha hizo ana laki moja tu, nilimwambia
awape.“Waliporudi na shilingi laki moja walisema nimewadanganya,
wakaniadhibu na kunivua nguo, wakanilawiti kwa zamu na kunilazimisha
kuwafanyia mambo ambayo ni tabu hata kuyasema huku wakinipiga picha.
“Baada ya kumaliza walichukuwa laptop, nguo na simu wakaondoka huku
wakiniambia ifikika Jumatatu, yaani siku moja baada ya tukio niwape
shilingi milioni moja la sivyo wanaweka picha zangu mtandaoni.
“Hata hivyo, baada ya kukosa hizo fedha waliziweka picha mtandaoni,
ikawa napigiwa simu na watu mbalimbali walioziona.“Waliponiacha pale
chumbani nikiwa sina nguvu, nilichukuwa shuka nilijikokota mpaka kwa
meneja wa gesti na kumweleza. Alinipa nguo yake ili niweze kwenda Kituo
Kidogo cha Polisi cha Minazi Mirefu kutoa taarifa na baadaye Buguruni
na kufungua kesi yenye jalada namba BUG/RB/8520/2014 Kujipatia Fedha kwa
Njia ya Udanganyifu lakini baadaye ikaongezwa shitaka lingine la
kulawiti.
“Kinachonishangaza ni kwamba iweje wanaume hao sita waingie na kutoka bila wenye gesti kuwabaini?” alihoji mwanaume huyo.
Naye mmiliki wa nyumba hiyo ya wageni alikiri kupokea taarifa ya
kutokea kwa tukio hilo na kudai kwamba ni la aibu na kusema suala hilo
linashughulikiwa na jeshi la polisi.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Ilala, SACP, Mary Nzuki alipohojiwa na
mmoja wa waandishi wa habari hii ofisini kwake mwishoni mwa wiki
iliyopita alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema tayari watuhumiwa
wanne wanashikiliwa Kamanda Nzuki aliwataja wanaoshikiliwa kuwa ni Erick
Kasila, Sanifa Sadik, Shela Sadik na Juma Richard
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment