KOCHA Patrick Phiri alipopata taarifa kuwamshambuliaji wao mpya Emmanuel Okwi ameruhusiwa kucheza Simba alishindwa kuzuia furaha yake na kutamka kuwa sasakazi imeanza rasmi.Straika namba moja wa Simba, Amissi Tambwe amefurahi kupita kiasi na kutamka kwamba: “Mmeniletea Okwi, mtaona kazi itakavyonoga.” Tambwe aliiambia Mwanaspoti kwamba: “Ni mchezaji mzuri ambaye ana kila sifa ya mshambuliaji kama tutashirikiana vizuri Simba itafika mbali sana na kila mtu atashangaa, tunajipanga kufanya kazi ya maana.”Tambwe alisema mchezaji huyo ni makini kutokana na aina yake ya uchezaji aliyoiona kuanzia siku za nyuma mpaka alipotua mazoezini Simba.Juzi Jumapili jioni Kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) chini ya Mwenyekiti wake Richard Sinamtwa ilipitia mkataba wa mchezaji huyo na kusikiliza hoja za pande zote mbili Yanga na Okwi na kubaini kwamba mkataba kati ya pande hizo ulivunjika kwa kukiuka kipengele cha 8 kinachohusu malipo ya usajili.Mpaka sasa Yanga ilimlipa Okwi Dola 50,000 (Sh 80 milioni kwa wakati huo) ya usajili huo na hivyo ikawa inadaiwa Dola 50,000 kwa makubaliano ya usajili wa Dola 100,000 (Sh 160 milioni kwa wakati huo) jambo ambalo lilipelekea mchezaji huyo kugoma kuichezea Yanga kwa madai kuwa mpaka amaliziwe fedha zake.Phiri alikuwa akifuatilia kwa karibu juu ya utata wa usajili wa mshambuliaji wake huyo ambaye Yanga walipinga usajili wakeSimba kwa madai kuwa bado ana mkataba na timu hiyo, huku Phiri akieleza kwamba angependa kuona Okwi anaichezea Simba kuliko kukaa bila kucheza kwani kipaji chake kingekufa.“Nafurahi sana kusikia Okwi ni mchezaji huru nami nitakuwa huru kumtumia katikakikosi changu, kwa kweli nimejawa na furaha kubwa kwa hilo, Okwi ni mchezaji mzuri na anapendwa na mashabiki wa soka nchini.“Tunarudi Zanzibar ambako nitalazimika kukaa na wachezaji wangu kwa ajili ya maandalizi ya Ligi Kuu ambayo naamini tutafanya vizuri, ila nitazungumza nao kuhusu umakini katika soka na kufanya juhudi katika ligi,” alisema Phiri.Okwi atangaza vitaOkwi aliiambia Mwanaspoti kwamba: “Nimefurahishwa na uamuzi huu wa TFF, nilijua kwamba kama wakizingatia ukweli na haki, nitawashinda Yanga na imekuwa hivyo, nawashukuru sana, sasa nataka kucheza mpira.”“Unajua nimepoteza muda mwingi katika kesi hizi mbalimbali, kwa mbali ni kama zilikuwa zinakimaliza kipaji changu sasa nataka kucheza mpira Simba, naomba watu waniache nicheze mpira nataka kurudi katika uwezo wangu,” alisisitiza Okwi. TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
LIKE PAGE YETU HAPO PIA SHARE STORY NA RAFIKI ZAKO

0 comments:

Post a Comment

BURUDANI

 
Top