Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji
ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imekutana leo (Septemba
7) na kupitia masuala mbalimbali ikiwemo mgogoro wa kimkataba kati ya
klabu ya Yanga na mchezaji Emmanuel Okwi.
Mkataba huo ulipitiwa na Kamati ikiwemo
kumsikiliza mchezaji mwenyewe pamoja na upande wa Yanga na kuridhika
kuwa mkataba kati ya pande hizo umevunjika Ukiwa ni mkataba wa pande
mbili Yanga ilikiuka kipengele namba 8 kuhusu malipo ya ada ya usajili.
Yanga ikiwa kama mwajiri haikutekeleza
kipengele hicho cha kimkataba hadi kufikia Juni 27 mwaka huu ilipoandika
barua TFF kuomba mkataba huo uvunjwe,Kwa maana hiyo Okwi ni mchezaji
huru,hivyo yuko huru kujiunga na timu yoyote.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment